• ePaper
Friday, May 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA APOKEA TUZO TELE ZA UTALII

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 6, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA APOKEA TUZO TELE ZA UTALII
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amekabidhiwa tuzo tatu kuu za utalii wa kimataifa, ambazo Tanzania imeshinda katika tuzo za Shirika la Utalii Duniani (WTA 2025), maarufu ‘World Travel Awards 2025’.

Tuzo hizo zilikabidhiwa kwa Rais na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ashatu Kijaji, kwa niaba ya wadau wa utalii katika hafla iliyofanyika, Ikulu ya Tunguu, Zanzibar.

Miongoni mwa tuzo hizo ni Tuzo ya Nchi Inayoongoza Duniani kwa Utalii wa Safari yaani ‘World’s Leading Safari Destination’, iliyotolewa katika kilele cha utoaji tuzo za utalii duniani zilizofanyika nchini Bahrain, Desemba 6, mwaka jana.

Washiriki wengine katika kipengele hicho ni Botswana, Kenya, Namibia, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ilitajwa kuwa hifadhi bora duniani kwa mwaka 2025, ikizitangulia hifadhi za Kruger ya Afrika Kusini na Yellowstone ya Marekani.

Tanzania pia ilishinda kuwa nchi inayoongoza kwa kutembelewa na watalii barani Afrika kwa mwaka jana wakati wa hafla ya kutunuku Tuzo za Dunia za Safari Afrika na Bahari ya Hindi, zilizofanyika Juni 28, 2025 jijini Dar es Salaam, ikishindanishwa na vivutio kadhaa vya juu vya utalii barani Afrika.

APONGEZA TAASISI ZA UTALII NCHINI

Rais Dk. Samia amezipongeza taasisi na wataalamu katika sekta ya utalii na uhifadhi kwa kulinda vivutio vya taifa na kuimarisha hadhi ya utalii wa kimataifa wa Tanzania.

Alisema mafanikio hayo yanaakisi upekee wa asili ya Tanzania, juhudi endelevu za uhifadhi na utangazaji wa kimkakati wa bidhaa za utalii.

Kwa mujibu wa Rais Dk. Samia, mafanikio hayo yanaakisi utajiri wa maliasili, wanyamapori, uhifadhi endelevu,  vyanzo vya maji, na ukarimu wa wananchi wake wanaovutia wageni kutoka mataifa mbalimbali.

Tuzo hizo zinathibitisha nafasi ya Tanzania kuwa nchi inayoongoza duniani kwa utalii unaozingatia asili na kusisitiza dhamira ya serikali katika uhifadhi na ushindani endelevu wa kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Zanzibar imeshinda tuzo ya Eneo Bora Afrika kwa Mikutano na Matukio ya Kitaasisi.

Ubora wa Tanzania ulionekana tena baada ya kuibuka mshindi wa tuzo za ‘World Travel Awards’,  ambapo Tanzania ilishinda jumla ya tuzo 45 katika Afrika, zikihusisha sekta za umma na binafsi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Pia, Tanzania ilipata tuzo mbili zaidi katika kundi la Sekta Binafsi, ikiwemo Kampuni Bora ya Safari za Puto Duniani, iliyotwaliwa na kampuni ya Serengeti Balloon Safaris na Kisiwa Bora cha Mapumziko Duniani na Jumaira Thanda Resort katika Kisiwa cha Mafia nchini Tanzania.

Tuzo za Wolrd Travel zilianzishwa 1993 zikiwa ni miongoni mwa tuzo zenye viwango vinavyoheshimika duniani katika sekta ya utalii.

Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), sekta hiyo ilipata ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na ongezeko la asilimia 9.02 la watalii kwa mwaka na kufikia 2,097,823 na kuweka rekodi ya kukusanya mapato ya dola za Marekani bilioni 4.2 mwaka jana, ikilinganishwa na dola bilioni 1.3 mwaka 2021.

Previous Post

‘PENALTI’ STARS YAIGAWA DUNIA

Next Post

‘UONGOZI SIYO HOTUBA ZENYE KUKONGA NYOYO BALI MATOKEO’

Next Post
‘UONGOZI SIYO HOTUBA ZENYE KUKONGA NYOYO BALI MATOKEO’

‘UONGOZI SIYO HOTUBA ZENYE KUKONGA NYOYO BALI MATOKEO’

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

‘TUMUOMBEE KARDINALI PENGO’

‘TUMUOMBEE KARDINALI PENGO’

4 months ago
TUZO YA CAF KWA RAIS DK. SAMIA NI HESHIMA

TUZO YA CAF KWA RAIS DK. SAMIA NI HESHIMA

6 months ago

Popular News

  • YANGA MBELE KWA MBELE

    YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?