• ePaper
Wednesday, March 11, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WACHINA WANAODAIWA KUKUTWA NA MABILIONI WAPANDISHWA KORTINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 7, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WACHINA WANAODAIWA KUKUTWA NA MABILIONI WAPANDISHWA KORTINI
0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na REHEMA MOHAMED

RAIA wawili wa China, wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka mawili ya kuongoza genge la uhalifu na kujipatia zaidi ya Dola la Marekani 707,075 (sawa na zaidi ya sh. bilioni 1.7) na sh. 281,710,000 kwa njia ya udanganyifu.

Weisi Wang na Yao Licong walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.

Wakili wa Serikali, Benjamin Muroto, akishirikiana na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita, alidai kati ya Desemba Mosi, 2024 hadi Desemba 30, mwaka jana, washitakiwa waliongoza genge la uhalifu.

Muroto alidai washitakiwa walitenda kosa hilo katika Mikoa ya  Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Kisiwani Unguja, Zanzibar na sehemu nyingine ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alidai Wang na Licong wakiwa maeneo hayo waliongoza genge la uhalifu kwa kutengeneza Kadi za Benki (ATM CARD) zenye taarifa za kughushi, kukwepa kodi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Pia, washitakiwa wanadaiwa katika tarehe na meneo hayo, kwa vitendo vyao walijipatia Dola za Marekani 707,075 na sh. 281,710,000, huku wakijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kuendesha genge la uhalifu.

Baada ya kusomewa mashitaka, Hakimu aliwaeleza washitakiwa kuwa hawapaswi kujibu lolote kwa ababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi, bali Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, upelelezi utakapokamilika.

Pia, aliwaeleza hawatapata dhamana kwa sababu shtaka la utakatishaji fedha halina dhamana, hivyo watapelekwa mahabusu.

Shauri hilo liliahirishwa hadi Januari 21, mwaka huu, kwa kutajwa.

Previous Post

REKODI MPYA ZANZIBAR

Next Post

BARKER, IBENGE VITA YA MBINU ‘MZIZIMA DERBY’

Next Post
BARKER, IBENGE VITA YA MBINU ‘MZIZIMA DERBY’

BARKER, IBENGE VITA YA MBINU ‘MZIZIMA DERBY’

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAMBO SAFI BIMA YA AFYA KWA WOTE

MAMBO SAFI BIMA YA AFYA KWA WOTE

3 months ago
NANAUKA AJA KIMKAKATI NEEMA YAZIDI KUWASHUKIA VIJANA

NANAUKA AJA KIMKAKATI NEEMA YAZIDI KUWASHUKIA VIJANA

2 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA AMUASILI MTOTO MCHANGA ALIYETELEKEZWA NZEGA

    RAIS DK. SAMIA AMUASILI MTOTO MCHANGA ALIYETELEKEZWA NZEGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SINGIDA, SIMBA BALAA ZITO LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MIGOGORO ARDHI MFUPA MGUMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MO DEWJI AIPAISHA TANZANIA KIMATAIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUHARAKISHA MABADILIKO KIDIJITALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?