• ePaper
Saturday, June 6, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RUNGU ZITO KUWASHUKIAWANAOTUNISHIANA MISULI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 4, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RUNGU ZITO KUWASHUKIAWANAOTUNISHIANA MISULI
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na IRENE MWASOMOLA, Manyara

KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amewaonya viongozi wa serikali na Chama wanaotunishiana misuli.

Amesisitiza kuwa, atakayefanya hivyo, atashughulikiwa katika vikao vya uamuzi.

Amesema kila mmoja aliyepewa dhamana, afahamu anamwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, hivyo wafanye kazi kwa umoja, ushirikiano na uadilifu mkubwa.

Kihongosi alisema hayo, alipozungumza na wanachama wa Shina Namba Nane, Tawi la Tunduru, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara.

Alisema viongozi wa Chama na serikali, wanatakiwa kufanya kazi kwa kushirikiana, hata zinapojitokeza fursa wafanye pamoja ili wananchi wafurahie maendeleo.

“Hatupaswi kutunishiana misuli au kuvimba kwa vyeo tulivyonavyo, tunachohitaji ni kazi, kama kuna mtu anaamini tunatania, afanye mambo isivyo aone, halafu tutakutana katika vikao vya uamuzi.

“Lazima kila mmoja aliyepewa dhamana afahamu anamwakilisha Rais Samia,” alisema. 

Kihongosi alisisitiza kuwa, CCM haihitaji kuona vurugu wala makundi katika maeneo yoyote ikiwemo Wilaya ya Simanjiro.

Aliwataka wananchi wa Simanjiro, kuhakikisha kipaumbele chao ni usalama wao, huku akiwataka kutokubali kushawishiwa kuharibu miundombinu ya nchi kwa maslahi ya watu.

Pia, aliwataka wananchi kutokubali kupandikizwa chuki ya kuvichukia vyombo vya usalama.

“Tusipandikizwe chuki kuhusu vyombo vyetu, amani ikitoweka hutafanya jambo lolote, lazima tudumishe umoja wa kitaifa, amani na upendo wa nchi yetu,” alisema. 

Kihongosi alisema CCM itabaki kuwa kimbilio la watu bila kubagua itikadi za dini, ukabila na ukanda katika kule maendeleo ya wananchi.

CAREN JOSEPH

Katibu wa Shina Namba Nane, Tawi la Tunduru,  Caren Joseph, alisema eneo hilo, lina wanachama 50, kati ya hao, wanawake 23 na wanaume 27.

Alisema wanaendelea kueneza siasa na itikadi za CCM katika eneo hilo na uhai wa Chama  kwa asilimia 100.

Previous Post

TANZANIA, RUSSIA KUPAISHA UCHUMI

Next Post

SERENGETI BOYS HESHIMA KILA KONA

Next Post
SERENGETI BOYS HESHIMA KILA KONA

SERENGETI BOYS HESHIMA KILA KONA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KWAHERI WILLIAM LUKUVI

KWAHERI WILLIAM LUKUVI

2 months ago
‘TUTAPELEKA MIRADI KWA WANANCHI WOTE’

‘TUTAPELEKA MIRADI KWA WANANCHI WOTE’

4 months ago

Popular News

  • MWANZA KINARA USIMAMIZI MAAFA

    MWANZA KINARA USIMAMIZI MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WFP KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA USIMAMIZI WA MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HESHIMA KUBWA KWA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU: MAMBO MAZURI YANAKUJA, AIPA TANO SERENGETI BOYS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERENGETI BOYS HESHIMA KILA KONA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?