• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KIHONGOSI AMWASHIA MOTO KIGOGO HOSPITALI MANYONI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 20, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KIHONGOSI AMWASHIA MOTO KIGOGO HOSPITALI MANYONI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SUPERIUS ERNEST

KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, ameagiza kuchukuliwa hatua Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manyoni, kufuatia malalamiko ya wananchi.

Kihongosi alimwagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Dk. James Bwire, kumchukulia hatua kufuatia malalamiko ya wananchi waliodai kutozwa gharama za matibabu nje ya utaratibu.

Kihongosi alitoa maagizo hayo katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi wa Itigi Wilaya ya Manyoni.

“Mfawidhi analalamikiwa sana, DMO hili liko ndani ya uwezo wako. Uwezo wa kumwondoa unao angalia kupitia utaratibu wako wa kazi, ulifanyie kazi kabla ya Januari 22 sijaondoka nipate ufafanuzi wa hatua ulizochukua, haiwezekani watu wanatakiwa kupata huduma wanatozwa fedha nje ya utaratibu hii haikubaliki,” alisema.

Katika hatua nyingine, Kihongosi alisisitiza watumishi wa umma kutekeleza wajibu kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Nafasi hizo mliziomba wenyewe, lazima mziheshimu muwatumikie wananchi kwa heshima na utiifu

“Vitendo vya watumishi kutowahudumia vyema wananchi, ndivyo vinachonganisha viongozi wa Serikali, Chama na wananchi,” alisema Kihongosi.

Akikagua Chuo Cha Veta Wilaya ya Manyoni ambacho kinaendelea na ujenzi, Kihongosi alimwagiza Mkuu wa Mkoa Halima Dendego, kutenga muda wa kuzungumza na wananchi na kutatua changamoto zao.

Previous Post

CCM INATEKELEZA AHADI KWA KASI – KIHONGOSI

Next Post

DEPU, OKELLO WAMOTO, YANGA IKISHINDA 6-0

Next Post
DEPU, OKELLO WAMOTO, YANGA IKISHINDA 6-0

DEPU, OKELLO WAMOTO, YANGA IKISHINDA 6-0

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA NA GHANA KUIMARISHA USHIRIKIANO KIUCHUMI NA AJIRA KWA VIJANA

TANZANIA NA GHANA KUIMARISHA USHIRIKIANO KIUCHUMI NA AJIRA KWA VIJANA

3 months ago
DK. MWIGULU ATUMA SALAMU KWA WALA RUSHWA, WAZEMBE

DK. MWIGULU ATUMA SALAMU KWA WALA RUSHWA, WAZEMBE

7 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?