Na AMINA KASHEBA
KOCHA wa Simba, Muafrika Kusini, Steve Barker amesema timu yake imeshindwa kuvuna pointi tatu dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na kushindwa kutumia vyema nafasi za wazi ilizozipata.
Simba ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar juzi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam, Barker alisema wachezaji wake walitengeneza nafasi nyingi, lakini walishindwa kuzibadili kuwa mabao.
“Tulitengeza nafasi nyingi za kufunga lakini wachezaji hawakufunga, hii ndiyo iliyowapa nguvu wapinzani kupambana hadi wakapata bao la kusawanzisha, tunakwenda kurekebisha makosa yaliyotokea,” alisema.
Kocha huyo alisema wanakwenda kujipanga kwa michezo ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Esperance de Tunis ya Tunisia.




