• ePaper
Wednesday, September 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI NA UMOJA WA ULAYA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 1, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
TANZANIA YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI NA UMOJA WA ULAYA
0
SHARES
23
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Umoja wa Ulaya kufuatia mafanikio ya ziara ya mashauriano ya ngazi ya juu yaliyofanyika Brussels, Ubelgiji yakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri Kombo alizungumza na viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya, wakiwemo, Makamu wa Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya na Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya wa Sera ya Mambo ya Nje na Usalama, Mheshimiwa Kaja Kallas, Kamati ya Kisiasa na Usalama ambayo ni jukwaa kuu la ngazi ya mabalozi la Umoja wa Ulaya kwa ajili ya uratibu wa sera za mambo ya nje, usalama na ulinzi; Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya, Mheshimiwa Younous Omarjee pamoja na Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Jozef Síkela.

Ushirikiano huu unaakisi mwelekeo wa diplomasia ya Tanzania yenye kujiamini, inayozingatia maendeleo, maslahi ya taifa, ushirikiano unaolenga matokeo, na ushirikiano wa kimataifa unaotekelezeka.

Akiambatana na Waziri wa Nchi kutoka Ofisi ya Rais, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri Kombo alifanya mashauriano ya kina na Kaja Kallas yaliyolenga kuimarisha ushirikiano wa vitendo kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, hususan katika maeneo ya amani na usalama wa kikanda, biashara inayozingatia utawala wa sheria, uwezeshaji wa uwekezaji, pamoja na mifumo thabiti na inayotabirika ya ushirikiano inayosaidia utekelezaji na ufanisi wa miradi.

Ziara hiyo ilijumuisha mashauriano na Kamati ya Kisiasa na Usalama (PSC) katika makao makuu ya taasisi kuu za Umoja wa Ulaya. Kamati hiyo, inayoundwa na Mabalozi wa Nchi Wanachama wote 27 wa Umoja wa Ulaya na kuongozwa na Balozi wa Urais unaohudumu wa Baraza la Umoja wa Ulaya, ndiyo chombo kikuu cha ngazi ya mabalozi kinachounda na kuongoza sera za mambo ya nje, usalama na ulinzi za Umoja huo.

Previous Post

WAZIRI MAVUNDE AZINDUA URUSHWAJI WA HELIKOPTA YA UTAFITI WA KINA WA MADINI

Next Post

ULEGA AAGIZA KUVUNJWA MKATABA WA MKANDARASI

Next Post
ULEGA AAGIZA KUVUNJWA MKATABA WA MKANDARASI

ULEGA AAGIZA KUVUNJWA MKATABA WA MKANDARASI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI YA DK. SAMIA KUIMARISHA UPATIKANAJI UMEME SONGWE

SERIKALI YA DK. SAMIA KUIMARISHA UPATIKANAJI UMEME SONGWE

1 year ago
SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI – DK. MWIGULU

SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI – DK. MWIGULU

3 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?