• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

GONCALVES: MECHI NA AS FAR RABAT NI FAINALI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 4, 2026
in Burudani, Kimataifa, Kitaifa, Michezo
0
GONCALVES: MECHI NA AS FAR RABAT NI FAINALI
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

BAADA ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly, kocha mkuu wa Yanga, Pedro Gonçalves amesema mechi na AS FAR Rabat  ni fainali kwao.

Kikosi cha Yanga kiliondoka nchini kuelekea Morocco kwa ajili ya mchezo wake wa tano wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FAR Rabat ya Morocco utakaopigwa Februari 7, mwaka huu katika Uwanja wa Stade Olympique, Rabat.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Pedro alisema wanakwenda nchini humo mapema ili kuzoea hali ya hewa ya huko na kupata muda mzuri wa kukijenga kikosi chake

“Mechi hiyo ni muhimu kwetu kuhakikisha tunapata ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo muhimu.

“Tumejipanga vizuri kuelekea katika mchezo huo, kwani tunaendea  kucheza kama fainali ya kufa au kupona, lengo letu ni kusonga mbele,” alisema Pedro.

Kocha huyo alisema hana hofu kwani anajivunia kuwa na wachezaji bora  ambao wana hali ya kujiamini na kupata matokeo.

MZIZE

Hata hivyo,  Pedro alisema kuwa nyota wake Clement Mzize tayari amerejea katika mazoezi na ndio wiki yake ya kwanza hivyo anaimani kubwa atakuwa vizuri katika mechi zinazofuata.

HERSI SAID

Rais wa klabu hiyo, Mhadisi Hersi Said alisema kikosi cha Yanga kinakwenda nchini humo kuhakikisha kinapambana kupata ushindi na kusonga mbele.

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu kwetu, lakini tutapambana mwanzo mwisho ili kupata matokeo mazuri,” alisema Hersi.

Naye Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kuwa wachezaji wanafahamu umuhimu wa mchezo huo, ana imani kuwa watapambana kupata ushindi.

Alifafanua kuwa wachezaji wanajua kuna raha ya kufuzu robo fainali hasa wakiwa ugenini.

 “Wachezaji wamekewa zawadi nono endapo watapata matokeo mazuri ugenini na kufanikiwa kutinga robo fainali ya mashindano hayo, tuna wachezaji wakubwa na wenye uwezo wa kutupa matokeo, sisi raha yetu ni kuona tunafuzu tukiwa ugenini,” alisema.

‎Kamwe alisema kuwa wana imani kubwa na kikosi chao kuwa kinaenda kuwapa raha mashabiki na wapenzi wa timu hiyo na Watanzania wote kwa jumla.

Kikosi kilichoondoka ni makipa, Djigue Diarra, Hussein Masagala, Abdultwalib Mshery, Israel Mwenda, Yao Kouassi, Ibrahim Bacca, Frank Assinki, Dikson Job, Chadrack Boka, Mohamed Hussein, Aziz Andambwile na Damaro Camara.

Wengine ni Duke Abuya, Lassine Kouma, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya, Allan Okello, Edmund John, Pacome Zouzoua, Emmanuel Mwanengo, Laurindo Aurelio ‘Depu’, Prince Dube na Clement Mzize.

‎Kwa sasa, msimamo wa Kundi B wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaongozwa na Al Ahly yenye pointi nane, ikifuatiwa na Yanga yenye pointi tano sawa na FAR Rabat huku JS Kabylie ikiwa na pointi 2.

Previous Post

NEEMA ZAIDI SEKTA KILIMO

Next Post

HATMA YA MANGUNGU BAADA YA SIMBA, ATLETICO

Next Post
HATMA YA MANGUNGU BAADA YA SIMBA, ATLETICO

HATMA YA MANGUNGU BAADA YA SIMBA, ATLETICO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NI MWANZO WA SIMULIZI MPYA

NI MWANZO WA SIMULIZI MPYA

4 months ago
DK. SAMIA APOKEA HATI ZA MABALOZI, ATEUA VIGOGO PSSSF, TANESCO 

DK. SAMIA APOKEA HATI ZA MABALOZI, ATEUA VIGOGO PSSSF, TANESCO 

4 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?