• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KIHONGOSI AANIKA UIMARA WA CCM KWA WATANZANIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 19, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KIHONGOSI AANIKA UIMARA WA CCM KWA WATANZANIA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI, Urambo

KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapindizi (CCM), Kenani Kihongosi, amesema Chama kitaendelea kuongoza kwa kuwa kinasimamia misingi ya demokrasia, utu na maendeleo.

Kauli hiyo aliitoa wakati akihitimisha ziara yake katika Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora na kusema CCM ndiyo Chama cha kuwaletea maendeleo Watanzania.

“Kuna baadhi ya watu wanasema Chama Cha Mapinduzi hakijafanya kitu si kweli, ukizungumzia umeme, maji, lami huwezi kusema bila kuitaja CCM,”alisema Kihongosi.

Aidha, alisema serikali imetumia sh. milioni 686 kujenga Kituo cha Afya cha Nsenda,  kusogeza huduma karibu kwa wanachi 18,998 wa vijiji vitano vya Kata ya Nsenda.

Alieleza CCM imeendelea kusimamia serikali katika utekelezaji wa Ilani yake hasa katika siku 100 za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akiwa madarakani.

Alisema ujenzi wa kituo hicho utakamilika Machi 30, mwaka huu ambapo hivi ujenzi umefikia asilimia 69.

Mradi wa Kituo Cha Afya Nsenda ulipokea sh. 686,135,134 kutoka serikali ukihusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la maabara, jengo la mama na mtoto, jengo la kufulia, vyoo vya nje na kichomea taka.

Ofisa Masuuli Mteule, Faid Chagula, alisema kituo hicho kitawanufaisha wananchi wa kata tano na kitapunguza vifo vya watoto wachanga na wajawazito.

“Kuna baadhi ya watu wanasema Chama Cha Mapinduzi hakijafanya kitu si kweli, ukizungumzia umeme, maji, lami huwezi kusema bila kuitaja CCM”

Kenani Kihongosi

Previous Post

‘TUTAPELEKA MIRADI KWA WANANCHI WOTE’

Next Post

SABABU ‘DABI’ YANGA, SIMBA KUPELEKWA Z’BAR

Next Post
SABABU ‘DABI’ YANGA, SIMBA KUPELEKWA Z’BAR

SABABU ‘DABI’ YANGA, SIMBA KUPELEKWA Z’BAR

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SINGIDA BS YAIPANIA SIMBA

SINGIDA BS YAIPANIA SIMBA

1 month ago
AHUKUMIWA KUNYONGWA KWA KUTIWA HATIANI KUUA

AHUKUMIWA KUNYONGWA KWA KUTIWA HATIANI KUUA

5 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?