• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MATOKEO YAMSIKITISHA KOCHA YANGA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 20, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
MATOKEO YAMSIKITISHA KOCHA YANGA
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

PAMOJA na kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cosmopolitan, Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves amesema amesikitishwa na uchache mabao machache yaliyopachikwa wavuni tofauti na nafasi walizotengeneza.

Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cosmopolitan katika mchezo wa hatua ya 64 bora ya Kombe la Shirikisho (FA), uliochezwa Uwanja wa KMC, Dar es Salaam na kutinga hatua ya 32 bora ya mashindano hayo.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kocha Pedro alisema timu yake bado imeendelea kuwa na tatizo la safu ya ushambuliaji na anahitaji kufanya marekebisho ya haraka ili kufanya vizuri zaidi katika mechi zinazofuata.

Alisema malengo yake ni kuona Yanga inafunga mabao mengi katika kila mchezo, hivyo atakwenda kuboresha na kuwapa mazoezi maalumu washambuliaji wake ili waweze kufunga mabao mengi.

 “Tumeshinda lakini sijafurahishwa na matokeo ambayo tumeyapata katika mchezo dhidi ya Cosmo, tumetengeneza nafasi nyingi na wachezaji wangu wameshindwa kuzitumia, hivyo ninahitaji kuboresha zaidi kikosi changu hasa nafasi ya ushambuliaji,” alisema Pedro.

Kocha huyo alisema kila mchezaji ana jukumu la kuipambania timu na kuhakikisha anatumia vyema nafasi anazozipata ili kuzibadilisha na kuwa mabao.

Pedro alisema anajivunia kikosi alichokuwa nacho kwani wachezaji wamekuwa wakionyesha kiwango kikubwa, lakini anahitaji kupata dawa ya washambuliaji wake ili kuzitumia nafasi wanazozipata kuwa mabao.

Hata hivyo, Pedro alizungumzia uwezo wa nyota wake mpya, Buba Jammeh ambaye alifunga mabao mawili katika mchezo huo kuwa ni mmoja wa wachezaji wenye kiwango cha hali ya juu na kwamba ataisaidia timu kufikia malengo.

“Namjua vizuri Buba, najua uwezo wake lakini kwa hivi sasa hayuko vizuri sana, yuko katika mchakato wa kurejea katika kiwango chake hivyo nina imani atakapokuwa vizuri ni msaada  mkubwa katika timu,” alisema Pedro.

Kocha huyo alisema pamoja na kupata ushindi lakini amekubali kiwango cha wapinzani wa Cosmopolitan kwani waliwaonyesha ushindani mkubwa.

Naye Buba alisema pamoja na kushinda mchezo huo bado hajaonyesha makali yake, hivyo anaamini atawafurahisha mashabiki katika mechi zitakazofuata.

Alisema huo ni mchezo wake wa kwanza kuichezea Yanga, ana furaha kuona mashabiki na wapenzi wa timu hiyo wamempokea vyema.

“Nimefurahi kuona nimeweza kusadia timu yangu katika mchezo wangu wa kwanza ikiwemo kupokelewa vyema na mashabiki, nitafanya mengi zaidi katika mechi zitakazofuata,” alisema.

Yanga inatarajia kuifuata Namungo, katika mchezo utakaofanyika Februari 22, mwaka huu ugenini kabla ya kurejea nyumbani kupepetana na JKT Tannzania, Februari 25, mwaka huu.

Previous Post

MANGUNGU AFUNGUKA SIMBA

Next Post

RAIS DK. MWINYI : HURUMA NA UADILIFU VIWE KIPAUMBELE MWEZI MTUKUFU

Next Post
RAIS DK. MWINYI : HURUMA NA UADILIFU VIWE KIPAUMBELE MWEZI MTUKUFU

RAIS DK. MWINYI : HURUMA NA UADILIFU VIWE KIPAUMBELE MWEZI MTUKUFU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MCHENGERWA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

MCHENGERWA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

2 months ago
SIMBACHAWENE AHIMIZA KUDUMISHA ZAIDI AMANI

SIMBACHAWENE AHIMIZA KUDUMISHA ZAIDI AMANI

6 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?