• ePaper
Saturday, May 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SIMBA, YANGA MZIGONI LEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 25, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
SIMBA, YANGA MZIGONI LEO
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

ZIKIBAKI siku nne kabla ya kuvaana, timu za Yanga na Simba leo zinashuka dimbani katika viwanja tofauti katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga inayonolewa na Kocha Pedro Goncalves itachuana na JKT Tanzania saa 10:00 jioni katika Uwanja wa KMC, Dar es Salaam wakati Simba ya Steven Barker ikicheza na Dodoma Jiji saa 1:15 usiku katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Baada ya mechi hizo, miamba hiyo ya soka nchini Jumapili hii itavaana katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar katika mchezo wa 11 wa Ligi Kuu Bara.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Kocha Barker alisema anajua mchezo dhidi ya Dodoma Jiji utakuwa mgumu lakini amekiandaa vyema kikosi chake kuvuna pointi tatu.

Barker alisema licha ya mechi hiyo kuwa ngumu, lakini hana wasiwasi kwani ana imani kubwa wachezaji wake watafanya kila linalowezekana kuvuna pointi tatu katika mtanange huo.

“Ninafahamu tunakwenda kukutana na mchezo mgumu lakini tumejipanga kucheza katika mpango wetu ili kuwa bora zaidi ya mpinzani na kutimiza malengo yetu ya kupata ushindi katika mechi hii,” alisema Barker.

Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, alisema mechi dhidi ya JKT Tanzania itakuwa ngumu lakini ana imani kikosi chake kitavuna pointi tatu katika mtanange huo.

Alisema wanapaswa kuwa tayari katika kila mchezo na kuonyesha uwezo waliokuwa nao kupata ushindi na kujizolea pointi tatu muhimu.

“Ukweli ni kwamba tuna muda mchache sana kujiandaa na mchezo ujao, tunapaswa kujiandaa vyema kuhakikisha tunapata matokeo licha ya changamoto ya muda wa kujiandaa, lakini sisi ni timu kubwa tunapaswa kukabiliana na kila kikwazo hasa katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania,” alisema.

Pedro alisema kuwa utakuwa mchezo mzuri na wamefanya maboresho machache katika maeneo yenye mapungufu kuhakikisha wanafanya vizuri.

Katika msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 25 huku Simba ikiwa nafasi ya nne kwa alama 22, kila moja ikishuka dimbani mara tisa.

Previous Post

DK. MWIGULU ATOA MAAGIZO AFCON 2027

Next Post

TAIFA STARS KUKIPIGA FIFA SERIES 2026

Next Post
TAIFA STARS KUKIPIGA FIFA SERIES 2026

TAIFA STARS KUKIPIGA FIFA SERIES 2026

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MRADI WA BILIONI 18.9/- BUKOBA WAMPA SIFA RAIS DK. SAMIA

MRADI WA BILIONI 18.9/- BUKOBA WAMPA SIFA RAIS DK. SAMIA

2 months ago
AL AHLY, YANGA UBORA UTAONGEA

AL AHLY, YANGA UBORA UTAONGEA

4 months ago

Popular News

  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASTAA YANGA WAUTAJA UBINGWA LIGI KUU BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?