• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

ATCL YARUDISHA WATANZANIA 236

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 9, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
ATCL YARUDISHA WATANZANIA 236
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na EMMANUEL MOHAMED

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL), limefanikiwa kuwarejesha nchini Watanzania 236 kutoka maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati waliokuwa wamekwama, baada mashirika ya ndege kusitisha safari zake kutokana na vita inayoendelea kati ya Marekani, Israel na Iran.

Akizungumza na UHURU jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Gervas Damas, alisema ndege hiyo iliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7:46 mchana.

Damas alisema ATCL ilipeleka ndege yake aina ya B787 Dreamliner ambayo iliondoka juzi usiku kwenda Dubai kuwachukua Watanzania waliokwama.

Alisema ndege hiyo ilirejea jana mchana kutokea Dubai na Watanzania hao waliokwama katika jiji hilo, baada ya mashirika ya ndege waliyokuwa wamekata tiketi kusimamisha huduma kutokana na kukosekana hali ya usalama Mashariki ya Kati kufuatia mapigano yanayoendelea.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ATCL machi 6, mwaka huu, ndege hiyo maalumu ilisafiri kwenda Dubai kuwafuata Watanzania waliokwama na kuwarejesha nchini.

ATCL ilisisitiza ndege hiyo haikuwa ya kibiashara, bali ilikwenda kutoa msaada wa kusafirisha wananchi hao.

Ndege zinazoingia na kutoka viwanja vya ndege vya Tel Aviv, Dubai, Doha na vituo vingine vya kimataifa katika eneo hilo zimesitisha kutoa huduma.

WIZARA YA MAMBO YA NJE

Aidha, taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki, iliwaomba watanzania kujisajili kupitia mfumo maalumu wa wizara kwa ufuatiliaji wa karibu na utaratibu wa kupata msaada wa kibalozi endapo ingehitajika kwa mtu yeyote aliyepata changamoto kutokana na mgogoro huo wa Mashariki ya Kati.

Pia, wizara ilielekeza kwa dharura watanzania walipaswa kuwasiliana na balozi za Tanzania zilizo katika miji ya Kuwait, Doha, Abu Dhabi, Ankara na Tel Aviv au Riyadh.

MACHI MOSI, 2026

Machi mosi, mwaka huu, Israel kwa kushirikiana na Marekani, zilianzisha mashambulizi dhidi ya Iran na kusababisha kifo cha kiongozi wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamenei.

Tangu tarehe hiyo hadi hivi sasa mapigano yamekuwa yakiendelea, hali iliyokwamisha raia wengi wa kigeni kurejea katika nchi zao kufuatia mashirika ya ndege kusitisha huduma za usafiri.

Previous Post

CELTIC, RANGERS WATIA AIBU

Next Post

WAZIRI MKUU AWAPA ‘TANO’ WANAOCHAPAKAZI SERIKALINI

Next Post
WAZIRI MKUU AWAPA ‘TANO’ WANAOCHAPAKAZI SERIKALINI

WAZIRI MKUU AWAPA ‘TANO’ WANAOCHAPAKAZI SERIKALINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWIGULU : POLISI WAACHE KUMTAFUTA ASKOFU GWAJIMA

DK. MWIGULU : POLISI WAACHE KUMTAFUTA ASKOFU GWAJIMA

5 months ago
DK. SAMIA AAHIDI FURSA ZAIDI KWA VIJANA NCHINI

DK. SAMIA AAHIDI FURSA ZAIDI KWA VIJANA NCHINI

7 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?