• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MIKOPO YA SERIKALI KWA VIJANA, FURSA MPYA KUKUZA UCHUMI WA UVUVI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 18, 2026
in Habari, Kitaifa, Makala
0
MIKOPO YA SERIKALI KWA VIJANA, FURSA MPYA KUKUZA UCHUMI WA UVUVI
0
SHARES
51
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

SERIKALI ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutoa mikopo ya masharti nafuu (isiyo na riba) kwa makundi mbalimbali ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Lengo la mikopo hiyo ya masharti nafuu ni kuwawezesha vijana kubuni miradi ya kiuchumi, itakayowaingizia kipato na kuboresha ustawi wa maisha yao, huku ikichochea ukuaji wa sekta muhimu za kiuchumi kama kilimo, mifugo na uvuvi ( ufugaji wa samaki kwa vizimba), badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini.

Hivi karibuni, serikali ilitoa mkopo wa sh. bilioni saba kwa vijana 308 kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwasaidia kuanzisha miradi ya uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji kupitia Programu ya Building a Better Tomorrow Youth Initiative (BBT – Uvuvi). Mpango huo unaonekana kuwa mkakati mpana wa serikali wa kuwainua vijana kiuchumi na kuongeza ajira nchini.

VIJANA WENGI, AJIRA CHACHE

Takwimu zinaonesha kuwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35, nchini wanafikia takribani milioni 20.6, sawa na zaidi ya theluthi moja ya Watanzania wote, kila mwaka takribani vijana milioni moja huhitimu mafunzo katika ngazi mbalimbali za elimu.

Hata hivyo, fursa za ajira rasmi hazitoshelezi mahitaji hayo. Kati ya vijana hao, ni takribani 40,000 tu wanaoajiriwa katika sekta ya umma na karibu 350,000 katika sekta binafsi.

Hali hii imeifanya serikali kubuni mbinu mbadala za kuwawezesha vijana kuanzisha miradi ya kiuchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa utoaji wa mikopo hiyo Machi 7, mwaka huu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, alisema mpango huo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia ya kutenga sh. bilioni 200, kuwawezesha vijana na makundi mbalimbali ya wajasiriamali.

“Tunataka vijana waone kuwa, fursa za ajira zipo katika sekta za uzalishaji mali, kupitia mikopo yenye masharti nafuu, vijana wanaweza kuanzisha miradi itakayowapatia kipato na kuchangia uchumi na maendeleo ya taifa,” alisema.

UVUVI KAMA INJINI YA AJIRA

Sekta ya uvuvi imeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha ajira na kipato kwa wananchi, hasa maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria na ukanda wa Bahari Kuu ya Hindi. Kwa mujibu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, sekta ya uvuvi inakua kwa wastani wa asilimia nne kwa mwaka na kuchangia takribani asilimia 1.8 ya pato la taifa.

Pia, alisema sekta hiyo imeajiri Watanzania 46,000 katika shughuli mbalimbali kuanzia uvuvi, usindikaji hadi biashara ya mazao ya samaki.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ng’wasi Kamani alisema kunan fursa katika uwekezaji miradi ya ufugaji wa samaki kwa vizimba na shughuli nyingine za ukuzaji viumbe maji.

Hali hiyo, itaongeza uzalishaji wa samaki na kuwapa vijana fursa ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi, hivyo uwekezaji katika teknolojia za kisasa za ufugaji samaki utaongeza uzalishaji na kukidhi mahitaji ya soko.

“Takwimu zinaonyesha uzalishaji wa samaki uko chini na ulaji wa samaki kwa mtu mmoja ni kilo 7.9 kwa mwaka, chini ya kiwango cha kilo 20 kinachopendekezwa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO).

Hivyo ipo fursa ya kuongeza uzalishaji wa samaki kufikia tani 559,199 kupitia ufugaji wa samaki katika  vizimba kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi,” alisema.

Kamani alisema, miradi hiyo itachangia kuongeza uzalishaji wa mazao ya uvuvi na wizara itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za mafunzo, benki na vituo vya ukuzaji viumbe maji kuhakikisha programu ya BBT, inaendelea kuwawezesha vijana wengi zaidi kujiajiri na kuchangia maendeleo ya taifa.

MAFUNZO NA UJUZI KWA VIJANA

Moja ya changamoto kubwa kwa vijana wengi wanaotaka kujiajiri ni ukosefu wa ujuzi wa vitendo na mitaji ya kuanzisha miradi.

Kupitia Programu ya BBT–Uvuvi, vijana wanapatiwa mafunzo ya kina yanayojumuisha mbinu za ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa majongoo bahari, kilimo cha mwani na unenepeshaji wa kaa.

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mohamed Ali Sheikh, vijana 500 walichaguliwa kuhudhuria  mafunzo ya vitendo yaliyofanyika katika vituo 15 vya ukuzaji viumbe maji vya serikali na binafsi kwa kipindi cha miezi mitatu.

Alisema, programu hiyo itaongeza ushiriki wa vijana katika shughuli za uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji  kuongeza uzalishaji wa mazao ya uvuvi  na kupunguza changamoto ya ajira.

“Vijana hao 486 walihitimu mafunzo hayo na sasa kati ya hao vijana 308 wanapatiwa mikopo kuanzisha miradi yao waliyoibuni wakati wa mafunzo. Utekelezaji wa programu hiyo umejikita maeneo makuu matatu ambayo ni mafunzo ya kubadili mtazamo wa vijana kuhusu kujiajiri, mafunzo ya vitendo kwa njia ya atamizi na uwezeshaji wa mitaji kupitia mikopo yenye masharti nafuu,” alisema.

Alifafanua kuwa, vijana 160 watatekeleza miradi ya ufugaji wa samaki kwa vizimba mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Simiyu, Geita na Kigoma, huku 48 wakitekeleza miradi ya ufugaji wa jongoo bahari, kilimo cha mwani na unenepeshaji wa kaa, katka mikoa ya Pwani na Mtwara.

MIRADI YENYE FAIDA KUBWA

Utafiti wa wataalamu wa sekta ya uvuvi unaonesha kuwa, ufugaji wa samaki kwa vizimba una faida kubwa kiuchumi endapo utaendeshwa kwa njia sahihi za kisasa.

Kwa mfano, kizimba kimoja kina uwezo wa kufuga vifaranga 11,500 vya samaki na kuzalisha wastani wa tani 3.5 za samaki katika kipindi cha miezi saba, ikiwa samaki hao watauzwa kwa wastani wa sh. 7,500 kwa kilo, mapato yanaweza kufikia zaidi ya sh. milioni 26 kwa mzunguko mmoja wa uzalishaji.

Baada ya kutoa gharama za uzalishaji, mwekezaji anaweza kupata faida ya zaidi ya sh. milioni tisa katika mzunguko huo wa kwanza, hali hiyo inaonesha kuwa sekta ya uvuvi ina uwezo mkubwa wa kuwainua vijana kiuchumi ikiwa itawekewa mazingira mazuri ya uwekezaji.

USHIRIKIANO WA TAASISI ZA FEDHA

Katika juhudi za kuimarisha uwekezaji katika sekta ya kilimo na uvuvi, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ( Tanzania Agricultural Development Bank-(TADB), imeendelea kutoa mikopo kwa vijana na wajasiriamali wanaojishughulisha na shughuli za uzalishaji mali kupitia sekta ya uvuvi.

Kaimu Mkurugenzi wa benki hiyo, Mkani Waziri alisema, katika kipindi cha miaka miwili benki hiyo imetoa mikopo yenye thamani ya sh. bilioni 14.07 kwa wanufaika 1,392 wanaojihusisha na ufugaji wa samaki kwa vizimba, kati ya wanufaika hao, vijana 577 sawa na asilimia 44 wamewezeshwa kuanzisha miradi yao katika mikoa ya Mwanza, Kagera, Geita, Simiyu, Mara na Kigoma.

“Katika kuchagiza maendeleo ya sekta ya kilimo na uvuvi, TADB inatekeleza miradi ya kimkakati ikiwa ni dhamira ya benki kuimarisha upatikanaji wa mitaji katika sekta hizo kuongeza uzalishaji, kukuza ajira kwa vijana, wanawake  na kuimarisha usalama wa chakula nchini,” alisema Waziri.

“Kwa miaka miwili kuanzia mwaka 2024 tumetoa mikopo ya sh. bilioni 14.07. Awamu ya kwanza zilitolewa boti na vizimba vya ufugaji wa samaki kwa wanufaika 1,392 kupitia vikundi 618.Miongoni mwa wanufaika hao, vijana 577 wamewezeshwa katika mikoa sita.”

Alieleza kuwa matokeo ya awali yanaonesha kuwa sh. bilioni 2.1 za mikopo isiyo na riba zimerejeshwa na vikundi 37, huku akiwataka wakopaji hao kuwa waaminifu katika kurejesha mikopo na wengine wanufaike.

CHANGAMOTO YA MAREJESHO YA MIKOPO

Pamoja na fursa zinazotolewa kupitia mikopo hiyo, serikali imeonya kuhusu umuhimu wa kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kurejeshwa kwa wakati.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda alisema, baadhi ya mikopo iliyotolewa hapo awali haikurejeshwa kutokana na wakopaji kutowajibika ipasavyo.

Alisema katika Wilaya ya Nyamagana pekee zaidi ya sh. bilioni tatu zilizowekezwa katika miradi mbalimbali bado hazijarejeshwa, jambo linalohitaji uwajibikaji na umakini mkubwa kutoka kwa wanufaika wa mikopo hiyo.

“Ilani ya CCM 2025-2030 imejipambanua kuwa ndani ya miaka mitano itawawezesha vijana. Fedha zinazowekezwa katika vizimba hazipotei.

Hata hivyo, hadi sasa Wilaya ya Nyamagana zaidi ya sh. bilioni 3 zilizowekezwa maeneo mengine hazijarejeshwa, wakopaji wamezima simu na hawapatikani. Hivyo suala la kuwapatia vijana fedha taslimu linapaswa kuangaliwa kwa umakini,” alionya.

Makilagi alisema serikali mkoani humo, itaendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa mapato ya ndani kupitia halmashauri zote za mkoa huo na  tayari Jiji la Mwanza limetenga sh. bilioni 1.8 kwa ajili ya vijana.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Dk. Semvua Mzigani, alisema wakala huo ndiyo watekelezaji wakuu wa mradi wa vijana wa BBT katika sekta ya uvuvi, wamejipanga kitaalamu kuusimamia, kuratibu na kuhakikisha unafanikiwa kwa viwango vinavyotakiwa.

Aliongeza kuwa wataweka miundombinu ya ufugaji wa samaki kwa vizimba, ni pamoja na upatikanaji wa vifaranga vya samaki na chakula cha samaki ya kufanikisha utekelezaji wa mradi huo.

FURSA YA KUKUZA UCHUMI WA BULUU

Serikali inaamini uwekezaji katika sekta ya uvuvi ni sehemu ya mkakati muhimu wa kukuza uchumi wa buluu wakati ambapo sasa, ulaji wa samaki nchini ni wastani wa kilo 7.9 kwa mtu kwa mwaka.

Alisema kiwango ambacho ni cha chini ukilinganisha na kiwango cha kilo 20 kinachopendekezwa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO).

Hiyo inaonesha kuwa bado kuna fursa kubwa ya kuongeza uzalishaji wa samaki nchini, kukidhi mahitaji ya soko la ndani na hata kuuza nje ya nchi, kupitia Programu ya BBT–Uvuvi, serikali inalenga kuwajengea uwezo vijana wa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali, kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa.

Kwa kufanya hivyo, vijana wanaweza kuwa sehemu muhimu ya mabadiliko ya kiuchumi nchini kwa kutumia rasilimali zilizopo kama maziwa, mito na bahari kuzalisha mali na kuboresha maisha yao.

Previous Post

TANZANIA ITAKAVYONUFAIKA KIUCHUMI, MKUTANO WA IPU

Next Post

MAELEKEZO YA SERIKALI KUHUSU USAFI NA UPANGAJI VIZIMBA KIVUTIO MUHIMU

Next Post
MAELEKEZO YA SERIKALI KUHUSU USAFI NA UPANGAJI VIZIMBA KIVUTIO MUHIMU

MAELEKEZO YA SERIKALI KUHUSU USAFI NA UPANGAJI VIZIMBA KIVUTIO MUHIMU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WASIRA ATABIRI RUNDO LA KURA KWA DK. SAMIA

WASIRA ATABIRI RUNDO LA KURA KWA DK. SAMIA

7 months ago
ALAMA TATU KUMUENZI JPM

ALAMA TATU KUMUENZI JPM

4 weeks ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?