Na MWANDISHI WETU
NI dhahiri. Mashabiki wa Yanga wamejikuta katika maumivu ya hali ya juu baada ya timu yao kushindwa kuvuna pointi tatu katika mchezo wa pili mfululizo katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Yanga imeshindwa kuvuna pointi hizo dhidi ya TRA United katika mtanange uliomalizika kwa sare ya bila kufungana katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Kikosi cha Kocha Pedro Goncalves ambacho kilicheza mchezo huo bila ya nyota wake Ibrahim Hamad Bacca, Dickson Job, Depu na Chadrack Boka, haikuwa katika ubora wake uliozoeleka kutokana na wapinzani wao kuonyesha ushindani wa hali ya juu katika kuzuia.
Katika mtanange huo ulioanza saa 10:00 jioni, TRA United ya Kocha Ettiene Ndayoragije, ilikuwa katika kiwango bora hasa safu ya ulinzi na kiungo, ikizuia vyema na kuanzisha vizuri mashambulizi dhidi ya safu ya ulinzi ya Yanga iliyoundwa na Bakari Mwamnyeto, Asinki, Mohamed Hussein na Israel Mwenda.
Mechi hiyo iliyokuwa na kasi ya aina ya, timu zote zilishambuliana kwa zamu na mara nyingi mashambulizi yalikuwa yakitengenezwa pembeni.
Katika dakika ya 78, Mzamiru Yassin wa TRA United alitolewa nje kwa kadi mbili za njano baada ya kumchezea rafu Tshabalala.
Awali dakika ya 36, Mzamiru alipewa kadi ya kwanza ya njano kwa kumchezea rafu Shekhan Rashid.
Licha ya kuwa pungufu, timu hiyo iliendelea kukaba kwa nidhamu na kutengeneza nafasi za kushambulia, lakini ilikosa umakini wa kufunga.
Baada ya suluhu hiyo, Yanga inaendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 37, baada ya michezo 15, huku TRA United ikishika nafasi ya 10 na kujizolea pointi 20 baada ya kushuka dimbani mara 15.
Kabla ya sare ya jana, Yanga ilitoka suluhu dhidi ya Azam FC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
TRA United: Jean Noel, Nasry Kombo, Valentin Nouma, Amy Mapaka, Karaboue Chamaou, Ramadhan Ramadhan, John Lazarus, Chande Chewe, Mzamiru Yassin, Jamali Dulaz na Joseph Akandwanaho.
Yanga: Djigue Diarra, Frank Assink, Bakari Mwanyeto, Maxi Nzengeli, Mohamed Damaro,




