• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAHITAJI YA UMEME YAONGEZEKA KWA WASTANI WA 10-15% KILA MWAKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 23, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
MAHITAJI YA UMEME YAONGEZEKA KWA WASTANI WA 10-15% KILA MWAKA
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

ONGEZEKO la idadi ya watu pamoja na kuimarika kwa shughuli za viwanda na biashara limeendelea kuchochea kasi ya mahitaji ya umeme nchini kwa wastani wa asilimia 10 hadi 15 kila mwaka.

Kutokana na mwenendo huo, Serikali imejipanga kuongeza jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wote, sambamba na kuimarisha miundombinu ya nishati.

Akizungumza katika mkutano wa Powering Africa Summit uliofanyika jijini Washington, DC, Machi 20, 2025, Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema kuwa ongezeko hilo la mahitaji linachochea uwekezaji mkubwa katika sekta ya nishati, ambayo ni mhimili muhimu wa ukuaji wa uchumi.

Amefafanua kuwa hadi kufikia Machi 2026, uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini umefikia megawati 4,383, wakati kiwango cha juu cha mahitaji kikiwa takribani megawati 2,100.

Hata hivyo, ameonya kuwa kasi ya ongezeko la mahitaji inahitaji uwekezaji zaidi katika uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme ili kuendana na mahitaji ya sasa na ya baadaye.

Kuhusu upatikanaji wa huduma hiyo, amesema Serikali imefanikiwa kufikisha miundombinu ya umeme katika vijiji vyote vya Tanzania Bara, ingawa kiwango cha uunganishaji wa umeme katika kaya bado ni cha chini, hali inayoonesha changamoto ya kuwafikia wananchi wote.

Salome amesisitiza kuwa Serikali imelenga kufikia asilimia 100 ya upatikanaji wa umeme ifikapo mwaka 2030, huku ikikusudia kuongeza kiwango cha uunganishaji wa kaya hadi asilimia 75 ili kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Aidha, ameeleza kuwa Tanzania ina vyanzo mbalimbali vya nishati ikiwemo gesi asilia, maji, jua, upepo na jotoardhi, ambavyo vina uwezo mkubwa wa kukidhi mahitaji yanayoongezeka.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuhimiza matumizi ya nishati jadidifu ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa umeme, huku ikiendeleza juhudi za kuhamasisha uwekezaji katika sekta hiyo.

Hatua hizo zinatarajiwa kusaidia kukidhi mahitaji ya nishati yanayoongezeka na kuiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha nishati katika ukanda wa Afrika.

Previous Post

TANZANIA MFANO BORA SEKTA YA MAJI DUNIANI

Next Post

USALITI WA UHUSIANO CHANZO CHA UKATILI

Next Post
USALITI WA UHUSIANO CHANZO CHA UKATILI

USALITI WA UHUSIANO CHANZO CHA UKATILI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

‘BODA BODA KWANGU NI ZAIDI YA KAZI INAYONIWEKA MJINI’

‘BODA BODA KWANGU NI ZAIDI YA KAZI INAYONIWEKA MJINI’

5 months ago
YANGA YATUMA SALAMU MSIMBAZI

YANGA YATUMA SALAMU MSIMBAZI

3 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?