• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SIMBA YATAKA KULIPA KISASI AZAM

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 29, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
SIMBA YATAKA KULIPA KISASI AZAM
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

UONGOZI wa klabu ya Simba umepania kuhakikisha wanalipa kisasi katika mchezo dhidi ya Azam FC, baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo zilipokutana.

Mchezo wa kwanza Simba dhidi ya Azam FC msimu huu ulichezwa Desemba 7 mwaka jana, Wekundu wa Msimbazi walikubali kichapo cha mabao 2-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Pia Simba ilipoteza bao 1-0 dhidi ya Azama, timu hizo zilipokutana kwa mara ya pili katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, mechi iliyofanyika Januari 8, mwaka huu.

Timu hizo zinatarajiwa kushuka dimbani Aprili 5, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa hawatakubali kuona wanarudia makosa waliyofanya mechi zilizopita, mchezo huo watahakikisha wanalipa kisasi.

Alisema wanajua Azam ni timu bora na wamewafunga katika mechi mbili zilizopita, lakini safari hii hawatakubali kuona wanapoteza.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu na wenye changamoto kubwa lakini hatutakubali kuona tunapoteza kwani tunahitaji ushindi ili kuweza kulipa kisasi,” alisema Ahmed.

Ahmed alisema kuwa hawana hofu na kikosi waliochokuwa nacho kwani Kocha Steve Baker anajua mapungufu ya kikosi, hivyo atafanya marekebisho ili kiweze kuwa bora na cha ushindani zaidi.

Alisema kuwa hawaiogopi Azam, pamoja na kupoteza mara mbili katika michezo yao na hivi sasa watahakikisha wanakwenda kuweka rekodi yao vizuri.

Ahmed alisema kuwa maandalizi kuelekea katika mchezo huo yanaendelea vizuri huku kocha akisubiria wachezaji wengine ambao wapo katika kikosi cha Taifa Stars.

Naye Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zacharia ‘Zaka za Kazi’ alisema kuwa wanataka kuendeleza historia yao ya kuifunga Simba.

Alisema anajua Simba hawatakubali kupoteza mchezo huo kwani kila mchezaji ana morari ya kutosha kuhakikisha anapambana mwanzo mwisho ili kupata ushindi.

“Tunajua hautakuwa mchezo mwepesi kwetu, tutapambana mwanzo hadi mwisho kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huo muhimu na kuendeleza historia yetu,” alisema Zaka.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 31 baada ya kushuka dimbani mara 14 huku Azam FC ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 29 baada ya kushuka dimbani mara 15.

Previous Post

GAMONDI AITOLEA MACHO MACAU

Next Post

WAZIRI MKUU : COCO BEACH HAIUZWI, NI YA WANANCHI

Next Post
WAZIRI MKUU : COCO BEACH HAIUZWI, NI YA WANANCHI

WAZIRI MKUU : COCO BEACH HAIUZWI, NI YA WANANCHI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NI MWANZO WA SIMULIZI MPYA

NI MWANZO WA SIMULIZI MPYA

4 months ago
WANNE ‘BYE BYE’ YANGA

WANNE ‘BYE BYE’ YANGA

4 months ago

Popular News

  • MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, MBEYA CITY KAZI IPO LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AFICHUA KUWA NA KIPAJI CHA SOKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?