• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAZIRI MKUU : COCO BEACH HAIUZWI, NI YA WANANCHI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 29, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAZIRI MKUU : COCO BEACH HAIUZWI, NI YA WANANCHI
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, ametoa ufafanuzi rasmi kuhusu hatma ya eneo la Coco Beach, akisisitiza kuwa halitauzwa kwa mwekezaji yeyote bali maboresho yatafanyika kwa manufaa ya wananchi waliopo katika eneo hilo.

Amesema hayo leo, Machi 29, 2026, alipotembelea eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam, ambapo alizungumza na wajasiriamali wadogo wanaofanya shughuli zao katika eneo hilo na kusikiliza kero zao mbalimbali.

“Coco Beach haiuzwi. La kwanza niwaondolee hofu—hapauzwi, wala hakuna mwekezaji mwingine zaidi yenu nyinyi wenyewe.

Hakuna atakayekuja kutoa maelekezo zaidi ya yale yaliyotolewa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Hapa hapauzwi,” amesisitiza.

Aidha, Dk. Mwigulu amesema Serikali itaendelea kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuhakikisha Watanzania wananufaika na maboresho yanayofanyika katika eneo hilo.

“Sisi wasaidizi wa Mheshimiwa Rais tutaendelea kuhakikisha Watanzania wanapata lile tabasamu la Mama ambalo amewaahidi,” amesema.

Katika hatua nyingine, Dk. Mwigulu amewataka watendaji wa Manispaa ya Kinondoni, akiwemo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri, Afisa Biashara pamoja na watendaji wengine, kubadili mtindo wa utendaji kazi kwa kuwafuata wananchi moja kwa moja badala ya kuwasubiri ofisini.

“Ninatoa agizo kwa Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Afisa Biashara pamoja na watendaji wengine—msikae ofisini tu. Tokeni mkazungumze na wananchi hawa moja kwa moja pale wanapokuwa na masuala yanayowahusu,” amesisitiza.

Kadhalika, Dk. Mwigulu amewahimiza wajasiriamali wa eneo la Coco Beach kuunga mkono juhudi za Serikali katika maboresho yanayoendelea kufanyika, huku akisisitiza kuwa fursa zitakazotokana na maboresho hayo zitawanufaisha wao wenyewe.

Previous Post

SIMBA YATAKA KULIPA KISASI AZAM

Next Post

RAIS DK. SAMIA ASISITIZA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI

Next Post
RAIS DK. SAMIA ASISITIZA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI

RAIS DK. SAMIA ASISITIZA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AKOSHA VIONGOZI WA KISIASA, DINI

RAIS DK. SAMIA AKOSHA VIONGOZI WA KISIASA, DINI

4 months ago
TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI GHARAMA NAFUU ZA BANDO

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI GHARAMA NAFUU ZA BANDO

3 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?