• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

KETE MUHIMU KWA YANGA LEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 28, 2025
in Burudani, Kitaifa, Michezo
0
KETE MUHIMU KWA YANGA LEO
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

YANGA leo itakuwa dimbani kusukuma kete yake muhimu dhidi ya JS Kabylie ya Algeria, kujiweka nafasi nzuri zaidi katika mbio za kuwania kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Timu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam, itachuana na Kabylie katika mechi ya pili ya kundi B la michuano hiyo itakayopigwa Uwanja wa Hocine Ait Ahmed, Tizi Ouzou nchini Algeria.

Katika mtanange huo utakaoanza saa 1:00 usiku, Yanga inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote kuweka sawa hesabu zake katika safari ya kutinga robo fainali kufuatia mechi ya kwanza dhidi ya AS Far Rabat ya Morocco, kushinda bao 1-0 nyumbani.

Akizungumzia mechi hiyo, Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, amesema ameiandaa vyema timu yake kuhakikisha inapata ushindi katika mtanange huo.

Pedro timu yake ipo vizuri na ina nafasi ya kupata ushindi.

Amesema anajua utakuwa mchezo mgumu lakini hawatakubali kuona wanapoteza.

 “Tumefanya mazoezi ya kutosha kuelekea katika mchezo huo, lengo letu kubwa ni kupata ushindi na kusonga mbele, tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini hatutakubali kurejea bila ya pointi tatu muhimu,” amesema Pedro.

Naye nahodha wa timu hiyo, Bakari Mwanyeto alisema wachezaji wamejipanga vyema kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.

“Ujue tunaingia katika mchezo mgumu, sisi kama wachezaji tumekaa kwa pamoja na kuelekezana kuhakikisha tunapata ushindi,” amesema Mwanyeto.

Katika kundi B, Yanga ipo pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, AS FAR ya Morocco na JS Kabylie ya Algeria.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA APONGEZWA UAMUZI SHEREHE ZA UHURU

Next Post

JKT YATAKATA LIGI KUU BARA

Next Post
JKT YATAKATA LIGI KUU BARA

JKT YATAKATA LIGI KUU BARA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MELI KUBWA NNE ZA MIZIGO KUIFUNGUA TANZANIA KIUCHUMI

MELI KUBWA NNE ZA MIZIGO KUIFUNGUA TANZANIA KIUCHUMI

1 month ago
KUVUMILIANA MUHIMU

KUVUMILIANA MUHIMU

2 days ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?