• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home AFYA

CHAI YA MOTO KUPITA KIASI YATAJWA KUCHOCHEA SARATANI YA KOO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 31, 2026
in AFYA, Habari, Kitaifa
0
CHAI YA MOTO KUPITA KIASI YATAJWA KUCHOCHEA SARATANI YA KOO
0
SHARES
15
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na EMMANUEL MOHAMED

UNYWAJI wa chai ya moto kupita kiasi pamoja na uji wa moto umetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazoweza kuongeza hatari ya kupata saratani ya koo.

Akizungumza na UHURUONLINE, Daktari Bingwa wa Saratani kutoka Hospitali ya Ocean Road, Dk. Sadiq Siu, amesema kuwa watu wengi wamezoea kunywa vinywaji vikiwa vya moto kupita kiasi, hali ambayo inaweza kuathiri afya ya koo.

Amesema joto kali linaweza kusababisha mabadiliko katika seli za ndani ya koo, jambo linaloweza kuchochea kuanza kwa saratani.

“Kinachotokea ni kuwa joto hilo husababisha seli za eneo husika kuanza kubadilika. Tukumbuke kuwa viungo vya ndani ya mwili hubadilika kwa haraka endapo vitapata athari,” amesema.

Dk. Sadiq ameongeza kuwa mabadiliko hayo ya seli yanaweza kuathiri utendaji wake wa kawaida na hatimaye kusababisha saratani.

“Tunapozungumzia saratani, tunazungumzia pia tabia hatarishi.

Miongoni mwa tabia hizo ni kunywa vinywaji vya moto kupita kiasi.

Kuna watu hadi chai lazima iwaunguze ndipo wanywe, hii si tabia salama,” amesema.

Aidha, ametaja mambo mengine yanayoongeza hatari ya kupata saratani ya koo kuwa ni matumizi ya tumbaku na ugoro.

Mbali na hilo, amesema ugonjwa huo pia unahusishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi, uvutaji wa sigara pamoja na unene uliopitiliza.

Previous Post

TAASISI ZINAZOFANYA VIBAYA KUANIKWA

Next Post

CHANETA IMANI KIBAO NA TUME HURU YA UCHUNGUZI

Next Post
CHANETA IMANI KIBAO NA TUME HURU YA UCHUNGUZI

CHANETA IMANI KIBAO NA TUME HURU YA UCHUNGUZI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AKOSHA VIONGOZI WA KISIASA, DINI

RAIS DK. SAMIA AKOSHA VIONGOZI WA KISIASA, DINI

4 months ago
DK. NCHIMBI AGUSIA UJIO WA FURSA ZA AJIRA

DK. NCHIMBI AGUSIA UJIO WA FURSA ZA AJIRA

2 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?