• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

CAG APENDEKEZA WIZARA MICHEZO KUIMARISHA USIMAMIZI WA UNUNUZI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 31, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
CAG APENDEKEZA WIZARA MICHEZO KUIMARISHA USIMAMIZI WA UNUNUZI
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MKAGUZI Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amependekeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, iimarishe usimamizi wa ununuzi kwa kuhakikisha makadirio yanayoaminika, matumizi sahihi ya njia za ununuzi na udhibiti madhubuti wa majadiliano na mabadiliko ya mikataba ili kulinda fedha za umma.

CAG Kichere aliyasema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam, alipowasilisha taarifa yake kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Alisema ripoti yake imebaini makadirio yasiyo sahihi ya gharama ya ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu uliopo Arusha na pia udhaifu katika majadiliano ya zabuni ya ujenzi wa uwanja huo unaotarajiwa kutumika katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027.

Kichere alisema kiwango cha fedha kilichotarajiwa kutumika katika ujenzi wa uwanja huo ni tofauti na kile kilichosainiwa katika mkataba wa ujenzi huo.

“Nilibaini mapungufu katika ununuzi wa mradi wa uwanja wa mpira wa Arusha wenye thamani ya sh. bilioni 338.54, hali inayoashiria kukosekana kwa thamani halisi ya fedha katika matumizi ya rasilimali za umma.

“ Kwanza, kulikuwa na tofauti kubwa kati ya makadirio na thamani ya mkataba, ambapo mradi ulikadiriwa kugharimu sh. bilioni 187, lakini ulisainiwa kwa thamani ya sh. bilioni 338.54 sawa na ongezeko la asilimia 81. Hali hii inaonyesha kuwa, makadirio hayakuwa sahihi na yaliathiri maamuzi ya kibajeti pamoja na utekelezaji wa mradi,” alisema.

Pia, CAG aliongeza kuwa: “Mkandarasi alipatikana kwa njia ya mzabuni mmoja (single source) kwa kisingizio cha dharura bila ya kuwepo ushahidi wa hali hiyo, ili kuondoa ushindani ambapo kungeweza kuhakikisha upatikanaji wa bei nafuu na kulinda maslahi ya serikali.

“Tatu, majadiliano ya zabuni yalifanyika kwa udhaifu ambapo sehemu kubwa ya vipengele vilivyojadiliwa havikuwa vimeidhinishwa kwenye mpango wa majadiliano na wigo wa kazi ulipunguzwa bila ya kupunguza gharama ipasavyo,”alisema.

Aidha, ali sema gharama zisizo halali ikiwemo  sh. bilioni 3.27 za gharama za zabuni zilijumuishwa katika mkataba na kubebwa na serikali.

“Kwa ujumla mheshimiwa Rais, hali hii inaonyesha udhaifu katika upangaji wa miradi, uteuzi wa wakandarasi na usimamizi wa majadiliano ya kimkataba, udhaifu huu unaweza kusababisha matumizi yasiyo na tija na kukosekana kwa thamani halisi ya fedha za umma,” alisema.

Previous Post

DK. MWIGULU MGENI RASMI MTOKO WA CHRISTINA SHUSHO

Next Post

SERIKALI KUENZI MEMA YA LUKUVI

Next Post
SERIKALI KUENZI MEMA YA LUKUVI

SERIKALI KUENZI MEMA YA LUKUVI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIMULIZI MAAJABU MIKOPO YA ASILIMIA 10

SIMULIZI MAAJABU MIKOPO YA ASILIMIA 10

7 months ago
MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

3 days ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?