• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA ATETA NA WAGOMBEA URAIS 2025

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 2, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA ATETA NA WAGOMBEA URAIS 2025
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akiitikia wito wao wa kufanya majadiliano ya pamoja kuhusu hali ya kisiasa na masuala ya maendeleo ya Taifa.

Viongozi hao kutoka vyama 16 vya siasa nchini, walimtembelea Rais Dk. Samia na kuwasilisha maoni yao kuhusu namna ya kuimarisha maridhiano ya kisiasa, demokrasia ya vyama, amani na mshikamano wa kitaifa baada ya uchaguzi mkuu na kuimarisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo na kudumisha tunu za umoja wa kitaifa.

YALIYOJADILIWA

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotumwa kwa vyombo vya habari, majadiliano hayo pia yaligusia umuhimu wa kuendeleza maadili ya uongozi, uwajibikaji na siasa zenye staha, kama msingi wa kujenga Taifa lenye utulivu wa kisiasa na maendeleo endelevu.

Katika kukuza demokrasia jumuishi, viongozi hao walisisitiza ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika masuala ya kitaifa na mchakato wa maendeleo.

Pia, kulinda utulivu wa kisiasa wakati wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo, kwa kutambua mazingira ya amani na umoja ni msingi wa ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.

Aidha, walielezea umuhimu wa kuimarisha utamaduni wa uvumilivu wa kisiasa, kuheshimiana na kujenga uaminifu miongoni mwa wadau wa kisiasa, kama njia ya kuendelea kudumisha utulivu wa nchi.

Kadhalika, walisisitiza umuhimu wa kuendeleza mazungumzo ya mara kwa mara baina ya viongozi wa kisiasa, ili kujenga uelewano wa pamoja na kushughulikia changamoto za kitaifa kwa njia ya mazungumzo na ushirikiano, kwa kutanguliza maslahi ya wananchi na maendeleo ya Taifa.

Mazungumzo hayo yanaakisi dhamira ya Rais Dk. Samia ya kuendeleza mawasiliano ya wazi ya kujenga miongoni mwa viongozi wa kisiasa kwa lengo la kuimarisha maridhiano na mshikamano wa kitaifa.

Previous Post

WADAU WAFICHUA AMANI INAVYOVUTIA WAWEKEZAJI

Next Post

DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

Next Post
DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MWENEZI KIHONGOSI NA MSISITIZO WA MAENDELEO, SIYO VURUGU

MWENEZI KIHONGOSI NA MSISITIZO WA MAENDELEO, SIYO VURUGU

2 weeks ago
MIILI YA WALIOFARIKI AJALI YA HELKOPTA YATAMBULIWA

MIILI YA WALIOFARIKI AJALI YA HELKOPTA YATAMBULIWA

4 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?