• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 2, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

SELINA MATHEW NA HAMIS SHIMYE DODOMA

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, ametoa maagizo 11 kwa viongozi wa serikali na taasisi nchini kutekeleza malengo na maono ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi.

Msimamo huo aliutoa jijini Dodoma, alipowasilisha Makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027, akisisitiza Rais Dk. Samia amedhamiria kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kasi kubwa.

Dk. Mwigulu alisema Serikali imedhamiria kuleta maendeleo na kutatua kero za wanachi kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na ufanisi katika kutekeleza bajeti ya ofisi hiyo kwa kutoa maagizo 11 kwa viongozi.

MAAGIZO

Alitaja maagizo hayo; ni kuanza utekelezaji wa Dira 2050 kupitia mpango na bajeti ulioandaliwa kwa kuhakikisha kila sekta inasimamia rasilimali za taifa maeneo yenye tija, matokeo makubwa na kupunguza utegemezi kutoka nje.

“Lengo ni kuishirikisha sekta binafsi na wadau wa maendeleo katika kuharakisha utekelezaji wa Dira 2050 ili kujenga uchumi jumuishi, shindani na unaotegemea uzalishaji wenye tija,” alisema.

Waziri Mkuu pia aliagiza,“Wakuu wa Mikoa wanapaswa kusimamia kikamilifu maandalizi na mapokezi ya wanafunzi wa elimu ya msingi ya lazima ya miaka kumi, watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2028, kwa kukamilisha miundombinu na huduma zote muhimu.”

Aigizo la tatu, Dk. Mwigulu alitaka kuimarishwa usimamizi wa makusanyo ya mapato kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na mashine za POS, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuziba mianya ya uvujaji wa fedha za umma na kuendeleza rasilimali fedha katika miradi ya kimkakati na kielelezo.

Dk. Mwigulu alisema agizo la nne ni wizara, taasisi na mamlaka zinazoshiriki katika uwezeshaji wananchi kiuchumi ziweke malengo yanayopimika, viashiria vya utendaji na ratiba za utekelezaji, kuhakikisha mitaji hiyo inazalisha ajira, kipato na biashara endelevu hasa kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, agizo la tano ni wakandarasi wanaotekeleza miradi ya Serikali watimize wajibu wao kwa mujibu wa mikataba waliyoingia, ikiwa ni pamoja na kuwalipa watoa huduma walioshiriki katika utekelezaji wa mradi husika.

“Maofisa masuuli kuhakikisha wazabuni na watoa huduma wanalipwa kwa wakati kwa mujibu wa makubaliano na huduma iliyotolewa,”alisema.

Agizo la sita, Waziri Mkuu aliwataka wakuu wa mikoa kuhakikisha ndani ya miezi sita baada ya kuanza utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2026/2027, wahakikishe shule zote katika halmashauri zina matundu ya vyoo kwa kuzingatia uwiano wa wanafunzi waliopo.

“Agizo la saba ni Wizara ya Maji; ihakikishe huduma ya maji inapatikana katika shule na vituo vyote vya kutolea huduma ya afya ndani ya miezi sita baada ya kuanza utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2026/2027. Baada ya muda huo, ni marufuku kwa wanafunzi kubeba maji na kupeleka shuleni,” alisema.

Waziri Mkuu Dk. Nchemba alisema agizo la nane ni ubora wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika sekta mbalimbali nchini, iwiane na thamani ya fedha iliyotolewa.

Alisisitiza; “Fedha zinazoelekezwa na Serikali kwenye miradi hiyo zitumike kama ilivyokusudiwa. Vilevile, wakandarasi wa ndani wawe wazalendo kwa kutumia ipasavyo fursa inayotolewa ya ushiriki wa kampuni zilizosajiliwa ndani kutekeleza miradi mikubwa.”

Waziri Mkuu alisema agizo la tisa; wizara za kisekta, taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa zilipe fidia kwa wananchi wanaopisha maeneo ya utekelezaji wa miradi ya Serikali kabla ya kutwaliwa kwa maeneo yao kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

 “Taasisi zote za umma ziimarishe ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali ikiwemo mipango, programu na miradi kuongeza tija ya utendaji kazi na kuboresha huduma kwa wananchi,” alisema.

Kwa upande wa agizo la 11, alizitaka wizara, mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, taasisi, wakala na idara zinazojitegemea kuanza kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi kama alivyoelekeza Rais.

AOMBA TRILIONI 12.5

Waziri Mkuu aliomba kuidhinishiwa jumla ya Sh trilioni 12.5, kwa ajili ya Ofisi yake na taasisi zilizo chini yake kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027, zikilenga kuimarisha uchumi na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Dk. Mwigulu alisema kati ya fedha hizo sh. trilioni 8.73 ni za matumizi ya kawaida, huku sh. trilioni 3.76 zikielekezwa katika miradi ya maendeleo.

Alisema pia, Serikali imeomba sh. bilioni 225.02 za Mfuko wa Bunge, kati ya hizo sh. bilioni 207.99 ni kwa matumizi ya kawaida na sh. bilioni 17.02 maendeleo.

Pia, alisema katika Mwaka wa Fedha 2026/27 ofisi hiyo inatarajiwa kukusanya maduhuli na mapato ya ndani ya jumla ya sh. trilioni 2.4.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA ATETA NA WAGOMBEA URAIS 2025

Next Post

PROFESA CHIJORIGA ACHAMBUA AMANI INAVYOLETA MAENDELEO

Next Post
PROFESA CHIJORIGA ACHAMBUA AMANI INAVYOLETA MAENDELEO

PROFESA CHIJORIGA ACHAMBUA AMANI INAVYOLETA MAENDELEO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIMBA, YANGA  ZAITA MASHABIKI

SIMBA, YANGA  ZAITA MASHABIKI

6 months ago
MAWAZIRI SABA NA MIKAKATI YA KAZI

MAWAZIRI SABA NA MIKAKATI YA KAZI

5 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?