• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SERA USIMAMIZI MALI ZA UMMA, KICHOCHEO CHA UKUAJI UCHUMI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 15, 2026
in Habari, Kitaifa, Makala
0
SERA USIMAMIZI MALI ZA UMMA, KICHOCHEO CHA UKUAJI UCHUMI
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeandika ukurasa mpya katika historia ya usimamizi wa mali na rasilimali za umma, baada ya kuzindua Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi ya mwaka 2025.

Sera hiyo iliyozinduliwa hivi karibuni na Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba kwa niaba ya Rais Dk. Samia ikiwa ni mageuzi ya kimfumo yanayolenga kuleta mabadiliko ya kina katika namna mali za umma zinavyosimamiwa.

“Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amenituma niwahakikishie serikali inaipa sera hii uzito unaostahili katika kuimarisha usimamizi wa rasilimali za taifa, kuongeza ufanisi katika usimamizi na matumizi ya fedha za umma, na kuchochea ukuaji wa shughuli jumuishi za kiuchumi nchini,” alisema.

Waziri Mkuu alisema kwa mara ya kwanza Tanzania inapata mwongozo mmoja wa kisera, unaounganisha hatua zote za mnyororo wa ugavi katika mtazamo jumuishi, kuanzia ununuzi, ugomboaji, upokeaji, uhifadhi, matumizi, usambazaji, urejeshaji hadi uondoshaji wa mali za umma.

Alisema uzinduzi huo ni hatua ya kimkakati inayodhihirisha dhamira ya serikali kujenga mifumo imara, yenye uwazi na inayowajibika kuhakikisha rasilimali za taifa zinasimamiwa kwa ufanisi.

Pia, kuleta tija kwa kuwa mwongozo mmoja wa kisera unaounganisha hatua zote muhimu za mnyororo wa ugavi katika mfumo jumuishi na unaoeleweka.

Kupitia sera hiyo, serikali inalenga kuondoa upungufu wa kiutendaji uliokuwa ukikwamisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Sera hiyo itaweka misingi ya uwajibikaji kwa watendaji, kuongeza nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kuhakikisha kila rasilimali inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Dk. Mwigulu alisema hatua itasaidia kuongeza imani ya wananchi kwa taasisi za umma na kuimarisha mazingira ya uwekezaji.

UMUHIMU WA SERA YA UGAVI

Waziri Mkuu alisema ni hatua muhimu inayoondoa mianya ya upotevu wa rasilimali, kupunguza urasimu na kuongeza tija katika utendaji wa taasisi za umma.

“Sera hiyo imekuja wakati ambapo mahitaji ya uwajibikaji na usimamizi madhubuti wa rasilimali yanaongezeka, sambamba na jitihada za serikali kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi,”alisema.

Alieleza kupitia utekelezaji wake, inatarajiwa kuimarisha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na kuhakikisha kila rasilimali ya taifa inaleta thamani inayokusudiwa.

Aidha, Waziri Mkuu alisema Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi ya mwaka 2025, ni chachu ya kujenga mifumo ya kisasa inayozingatia teknolojia na ubunifu katika usimamizi wa ugavi, hivyo kuweka msingi imara wa uchumi endelevu na shindani.

Waziri Mkuu alisema sera hiyo inaweka mkazo katika matumizi ya malighafi na wataalamu wa ndani, kukuza viwanda vya ndani, kuimarisha miundombinu ya kiteknolojia na kuzingatia hifadhi ya mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Kwa kufanya hivyo, mnyororo wa ugavi umeimarishwa kuwa chombo cha kimkakati cha kuongeza uzalishaji na ugavi wa bidhaa na huduma, uendelevu na ushindani wa taifa katika masoko ya kikanda na kimataifa,” alisema Waziri Mkuu.

Alisema zaidi ya asilimia 50 ya matumizi ya serikali hufanyika hupitia shughuli za ununuzi wa bidhaa na huduma, ikiwa ni sehemu muhimu ya shughuli za mnyororo wa ugavi.

Alisema hatua hiyo inaonesha kuwa uimara wa mfumo huo, una athari ya moja kwa moja katika usimamizi wa fedha za umma, ukuaji wa uchumi, upatikanaji wa bidhaa na huduma bora kwa wananchi.

Alisema serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuimarisha usimamizi wa shughuli za ununuzi wa Umma na Ugavi ikiwa ni pamoja na kutungwa na kutumika kwa Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 10 ya Mwaka 2023 na kuanzishwa mifumo ya TEHAMA kama NeST, TANCIS, GIMIS na MUSE ili kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika hatua za mnyororo wa ugavi.

Waziri Mkuu alisema kupitia utekelezaji wa sera hiyo, serikali inalenga kuendelea kuimarisha matumizi ya TEHAMA kupunguza mianya ya upotevu wa rasilimali za umma, kuongeza ufanisi katika usimamizi wa shughuli za serikali na kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma za Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa.

UMUHIMU WA SEKTA BINAFSI

Sekta binafsi imeendelea kuwa injini muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini, hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inashuhudia mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kiteknolojia na kiushindani.

Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 imeweka mkazo wa kimkakati katika kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuiwezesha sekta binafsi kukua, kushindana na kuchangia kwa kiwango kikubwa zaidi katika uchumi wa taifa.

Waziri Mkuu alisema sekta binafsi ina nafasi kubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hivyo Dira 2050 inalenga kuiwezesha sekta hiyo kuwa imara na shirikishi ili kuendeleza uvumbuzi, ubunifu na ukuaji endelevu.

Dira hiyo pia inalenga kufanya mabadiliko na mageuzi makubwa katika sekta binafsi huku ikitoa fursa sawa za kiuchumi kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

“Nimefurahi kusikia sera hii imeandaliwa kwa utaratibu wa ushirikishaji mpana wa wadau na kuzingatia kikamilifu malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mwelekeo wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2025 – 2030. Kupitia sera hii, sekta binafsi inatambuliwa rasmi kama mdau wa kimkakati wa serikali katika usimamizi wa mnyororo wa ugavi,”alisema.

Dk. Mwigulu alisema makundi maalumu ya kijamii, wakiwemo vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu, wamewekewa mazingira mahsusi ya uwezeshaji ili kuongeza ushiriki wao katika hatua mbalimbali za ugavi wa bidhaa na huduma.

KAULI YA WAZIRI WA FEDHA

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omar, alisema pamoja na jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali bado fedha nyingi za umma zinapotea kupitia udhaifu katika usimamizi wa mnyororo wa ugavi.

Balozi Omar alisema bado kuna upendeleo katika ununuzi na uondoaji wa mali, kuna udanganyifu mkubwa katika gharama za manunuzi, ikiwemo miradi ya maendeleo.

“Bado kuna rushwa katika usimamizi wa mnyororo wa ugavi katika sekta ya umma. Zikisimamiwa vyema, fedha chache tulizonazo zinaweza kutufikisha mbali katika kuhudumia wananchi na kuimarisha maendeleo,” alisema.

Alisema sera iliyozinduliwa imelenga kuimarisha mfumo wa mnyororo wa ugavi katika sekta ya umma, kurahisisha upatikanaji wa mahitaji ya serikali kwa ubora unaostahili, kupata thamani halisi ya fedha, kurahisisha taratibu za ugomboaji na uondoshaji wa mizigo ya Serikali; kuimarisha mifumo ya upokeaji na urejeshaji wa mali na kuimarisha utunzaji, uhifadhi, matumizi na usambazaji wa bidhaa na mali za umma.

“Kuimarisha misingi ya utawala bora na utawala wa sheria katika ununuzi wa umma na ugavi ikiwemo kudhibiti vitendo vya upendeleo, rushwa na mifumo ya hifadhi ya mazingira

“Pia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuitambua sekta binafsi kama nguzo ya kimkakati na wadau wa ndani kama fursa ya kumiliki njia kuu za kiuchumi,” aliongeza Waziri Mkuu.

Waziri huyo alitaja lengo jingine la sera hiyo ni kuweka mazingira wezeshi kwa kampuni za ndani na makundi maalumu ya kijamii, kushiriki kikamilifu shughuli za mnyororo wa ugavi kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi kuongeza mnyororo wa thamani.

Previous Post

UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

Next Post

MUOSHA MAGARI AAMRIWA KUFANYA USAFI MAHAKAMANI

Next Post
MUOSHA MAGARI AAMRIWA KUFANYA USAFI MAHAKAMANI

MUOSHA MAGARI AAMRIWA KUFANYA USAFI MAHAKAMANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MIGIRO KATIBU MKUU WA  KWANZA MWANAMKE NA MIKAKATI YA KUIMARISHA MASHINA KATIKA MITAA

MIGIRO KATIBU MKUU WA  KWANZA MWANAMKE NA MIKAKATI YA KUIMARISHA MASHINA KATIKA MITAA

3 months ago
KIHONGOSI AFICHUA SIRI MIKUTANO YA MGOMBEA URAIS CCM ‘KUFURIKA’

KIHONGOSI AFICHUA SIRI MIKUTANO YA MGOMBEA URAIS CCM ‘KUFURIKA’

7 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?