• ePaper
Monday, June 29, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KIHONGOSI AKEMEA ‘WANAOVIMBA’ CCM

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 14, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KIHONGOSI AKEMEA ‘WANAOVIMBA’ CCM
0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Musoma

Na IRENE MWASOMOLA

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amesema hakuna mkubwa kuliko Chama.

Amesema endapo Chama kikibaini kuna mtu anataka kukiharibu, kitamshughulikia bila kujali umaarufu wala cheo alichonacho.

Aidha, amesisitiza kuwa CCM itaendelea kulinda hadhi yake, hivyo asitokee mtu akajiona mkubwa kuliko Chama na kwamba kina misingi imara inayoendelea kusimamiwa tangu kilipoasisiwa.

Kihongosi alieleza hayo alipokuwa akizungumza na wanachama wa Shina Namba Tano, Kata ya Mwisenga, mjini Musoma mkoani Mara, ambapo aliwataka viongozi kuanzia ngazi ya shina kuendelea kuweka maslahi ya Chama mbele na siyo ya mtu binafsi.

Alisema CCM ni taasisi siyo mali ya mtu, hivyo vyama vingine vijifunze kwa sababu vipo ambavyo kiongozi mmoja akiondoka navyo vinakufa.

“Asije akatokea mtu akajiona yeye ni mkubwa kuliko Chama, anajidanganya kwa kuwa Chama hiki kina misingi na utaratibu tangu kilipoasisiwa.

“Chama hakijawahi kukosea hata siku moja, uamuzi wa Chama lazima uheshimiwe na watu wote, hakuna mkubwa kuliko CCM na ukitaka kuamini hilo wewe ondoka katika uongozi wa Chama kuwa raia wa kawaida uone kama utakuwa na heshima, heshima yako ni kwa sababu ya Chama Cha Mapinduzi,” alisema.

Pia, alisema Chama kikijua mtu anataka kuharibu kitamshughulikia bila kujali umaarufu na cheo alichonacho.

Vilevile, Kihongosi aliwataka viongozi wa CCM ngazi zote kulinda heshima na hadhi ya Chama kwa mienendo mbele ya wanaowaongoza.

Alisema CCM itabaki kuwa Chama kiongozi mkoani Mara na taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Kihongosi, amekwenda mkoani Mara kuona fedha zinazotolewa na serikali zimefanya kazi gani na kwamba hiyo ndiyo kazi ya Chama.

Pia, aliwataka wana CCM kuendelea kushiriki vikao vya mashina, kuishi kwa upendo, umoja na mshikamano.

“Vikao vya Chama viwe ajenda endelevu, tuendelee kuvifanya, pia wana CCM na Watanzania wote tuendelee kuishi kwa umoja na mshikamano,” alisisitiza.

Awali, Katibu wa Shina Namba Tano, Kata ya Mwisenga, Emiliana Kuboja, alisema shina hilo lina wanachama 50 na kati yao 35 wameshalipa ada ya uanachama.

Emiliana alisema shina hilo linajivunia mafanikio mbalimbali ikiweko kushinda uchaguzi kwa kishindo nafasi zote ukiwemo ubunge, udiwani na urais.

Daud Magabe mkazi wa eneo hilo, alisema wanakabiliwa na kero ya ubovu wa barabara ikiwemo inayokwenda katika Shule ya Msingi Mwisenga, aliyosoma Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema mwaka 2019 serikali iliahidi kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami, lakini ahadi hiyo bado haijatimia.

Kihongosi yupo mkoani Mara kwa ziara ya siku nne ambayo ilianza jana na inatarajiwa kuhitimishwa Mei 17, mwaka huu.

Ziara hiyo imelenga kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, kuangalia uhai wa Chama kuanzia ngazi ya shina na kutembelea miradi ya maendeleo.

Previous Post

MARUFUKU KUZUIA WANAFUNZI MITIHANI KISA ADA – DK. MWIGULU

Next Post

NEEMA YAWASHUKIA WAVUVI NA WAFUGAJI

Next Post
NEEMA YAWASHUKIA WAVUVI NA WAFUGAJI

NEEMA YAWASHUKIA WAVUVI NA WAFUGAJI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIFA KEMKEMU ZA LUKUVI

SIFA KEMKEMU ZA LUKUVI

3 months ago
EDNA LEMA AWAITA MASHABIKI KMC

EDNA LEMA AWAITA MASHABIKI KMC

6 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA AVUTIA UWEKEZAJI WA TIJA

    RAIS DK. SAMIA AVUTIA UWEKEZAJI WA TIJA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HAKUNA MJADALA AMANI, USALAMA WA NCHI-MWIGULU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VIJANA 400  WAAGWA KWENDA KUFANYA KAZI NJE YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘NAFUU YA MAFUTA KUANZA KUONEKANA JULAI’ NDEJEMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?