• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

KOCHA SERENGETI BOYS AFUNGUKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 26, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
KOCHA SERENGETI BOYS AFUNGUKA
0
SHARES
15
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

PAMOJA na Tanzania kufuzu nusu  fainali katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika , Kocha wa timu ya taifa kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Elieneza Nsanganzelu,  amedai kuwa  mchezo  dhidi ya Algeria ulikuwa na upinzani mkubwa.

Serengeti Boys ilishinda kwa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya Algeria, baada ya timu hizo kutoka sare 3-3 ndani ya dakika 90, katika mtanange uliopigwa Uwanja wa Mohammed XVI, Rabat nchini Morocco.

Kutokana na matokeo hayo, Serengeti Boys itaumana na Misri katika mechi ya nusu fainali kutafuta nafasi ya kucheza  fainali.

Nsanganzelu alisema katika mchezo huo, kikosi chake kilikabiliwa na upinzani mkali uliotokana na kiu ya kuitoa Tanzania ambayo ni timu tishio katika mashindano.

“Ilikuwa mechi ambayo wapinzani nao walitaka ushindi, pamoja na Algeria kuwa na vijana wengi wanaocheza soka barani Ulaya, wachezaji wangu walijipanga kuwaonyesha kuwa ni bora zaidi yao,” alisema.

Kocha huyo alisema baada ya kusonga mbele, anajua kuwa mchezo wa nusu fainali utakuwa mgumu zaidi lakini anaiandaa timu kupata matokeo mazuri zaidi na kucheza fainali.

 “Tunaenda  kufanyia kazi kasoro zote zilizojitokeza katika mechi za makundi na robo fainali, sasa mguvu zote tumeelekeza katika mchezo wa nusu fainali,” alisisitiza.

Nahodha wa Serengeti Boys, Kassim Juma, alisema mechi ilikuwa ngumu kwani Algeria ilitoa upinzani mkali.

Mchezaji huyo aliwaomba Watanzania kuendelea kuwasapoti kwani hatua ya nusu fainali waliyofikia ni kubwa tofauti na walipotoka, wanahitaji maombi kwa ajili ya kufika fainali.

“Haikuwa kazi nyepesi ni kitu cha kujitolea kwa sababu wapinzani walijipanga kuhakikisha wanashinda, lakini sisi tulisikiliza maelekezo ya walimu wetu,” alisema.

Serengeti  Boys tayari imeshafuzu kucheza michuano ya fainali za Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar kuanzia Novemba 19 hadi Desemba 13, mwaka huu baada ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

Previous Post

MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

Next Post

KOCHA SIMBA ACHEFUKWA

Next Post
KOCHA SIMBA ACHEFUKWA

KOCHA SIMBA ACHEFUKWA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SALUM ATHUMAN SALUM, JEMBE LA KMC LENYE UCHU WA KUCHEZA SOKA ULAYA 

SALUM ATHUMAN SALUM, JEMBE LA KMC LENYE UCHU WA KUCHEZA SOKA ULAYA 

8 months ago
RAIS DK. SAMIA ABADILI MATUMIZI YA FEDHA

RAIS DK. SAMIA ABADILI MATUMIZI YA FEDHA

3 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?