• ePaper
Tuesday, May 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NEEMA YA AJIRA MAMBO YA NDANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 26, 2026
in Habari, Kitaifa
0
NEEMA YA AJIRA MAMBO YA NDANI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH, Dodoma

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imetangaza kumwaga ajira 10,919 kwa Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Makao Makuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Pia, inatarajia kuwapandisha vyeo watumishi 23,089 ambapo kati ya hao, watumishi 73 kutoka Makao Makuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Polisi 13,487, Jeshi la Magereza 6,579, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 833, Idara ya Uhamiaji 2,028 na NIDA watumishi 89.

Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini hapa jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alisema ajira na upandishwaji vyeo hivyo ni katika mwaka wa fedha 2026/2027.

“Katika mwaka 2026/27, Wizara inatarajia kuajiri watumishi 10,919. Kati ya hao, watumishi wa Makao Makuu ya Wizara 249, Jeshi la Polisi 8,040, Jeshi la Magereza 1,046, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 500, Idara ya Uhamiaji 1,000 na NIDA 84,” alisisitiza.

UPANDISHWAJI VYEO

Kwa mujibu wa Patrobas, serikali imeendelea kupandisha vyeo watumishi wa wizara hiyo, kwa kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili mwaka huu, watumishi 9,689 wamepandishwa vyeo.

Alisema makao makuu ya wizara watumishi 106, Jeshi la Polisi 5,539, Jeshi la Magereza 3,220, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 75, Idara ya Uhamiaji 693 na NIDA 56.

Alibainisha kuwa katika mwaka 2026/27, wizara hiyo inatarajia kuwapandisha vyeo watumishi 23,089, Makao Makuu ya wizara 73, Jeshi la Polisi 13,487, Jeshi la Magereza 6,579, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 833, Idara ya Uhamiaji 2,028 na NIDA 89.
“Katika mwaka 2026/27, wizara imetenga sh. bilioni 38.81 kuwezesha mafunzo kwa watumishi 23,547. Kati ya hao, watumishi wa Makao Makuu ya wizara 85, Jeshi la Polisi 15,508, Jeshi la Magereza 3,500, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 1,508, Idara ya Uhamiaji 2,789 na NIDA 157.

Aliongeza: “Katika kuboresha utendaji kazi, wizara imewezesha upatikanaji mafunzo kwa watumishi 13,475 ndani na nje ya nchi. Kati ya hao, Makao Makuu ya wizara watumishi 172, Jeshi la Polisi 8,457, Jeshi la Magereza 2,030, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 1,358, Idara ya Uhamiaji 1,324 na NIDA 134.”

MAKOSA MAKUBWA YA JINAI YAPUNGUA

Katambi alibanisha kuwa, katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili mwaka huu, makosa makubwa ya jinai yaliyotolewa taarifa katika vituo vya polisi yalikuwa 39,027 ikilinganishwa na makosa 40,022 yaliyotolewa taarifa katika kipindi kama hicho mwaka 2024/25.

Alisema kuwa, kupungua makosa hayo kumesababishwa na kuongezeka uelewa na ushirikiano wa jamii katika
kubaini na kuzuia uhalifu.

“Kati ya makosa hayo 9,603 ni makosa dhidi ya binadamu, 13,986 makosa dhidi ya maadili ya jamii, 14,794 makosa ya kuwania mali na 644 makosa ya uhalifu wa kifedha,” alisisitiza.

MAKOSA YA KIMTANDAO YAONGEZEKA

Waziri huyo, alisema katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili mwaka huu makosa ya uhalifu wa kimtandao yaliyotolewa taarifa katika vituo vya polisi, yameongezeka kutoka 748 mwaka 2024/25 hadi 1,323.

Alisema idadi ya makosa hayo imeongezeka kutokana na askari kutumia vifaa vya kisasa vya uchunguzi, kufanya operesheni, doria mtandaoni na mwitikio chanya wa wananchi kutoa taarifa kuhusu uhalifu wa mtandao.

Katambi alisema wizara kupitia Jeshi la Polisi itaendelea kudhibiti uhalifu wa kimtandao ikiwemo matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na udukuzi wa taarifa za kimtandao kwa kuanzisha ofisi za kanda za upelelezi wa makosa ya uhalifu wa kimtandao katika Jiji la Dodoma na Zanzibar.

Pia, alisema imeweka mifumo ya ufuatiliaji wa shambulio la kimtandao, kuimarisha kikosi maalum cha kudhibiti taarifa potofu na uchochezi mtandaoni, kutoa elimu kwa umma kuhusu athari za kusambaza taarifa za uongo, kufuatilia na kudhibiti akaunti hatarishi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

MADEREVA MILIONI TATU WAKIUKA ZA USALAMA SHERIA BARABARANI

Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), alisema wizara kupitia Jeshi la Polisi, imeendelea kudhibiti makosa ya usalama barabarani yanayosababisha vifo na majeruhi kwa kufanya doria katika barabara mbalimbali nchini.

Kupitia doria hizo, alisema jumla ya madereva 3,051,541 waliokiuka sheria za usalama barabarani walikamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kuwapa onyo, kuwatoza faini, kuwafikisha mahakamani na kuwafungia leseni.

Vilevile, alisema jeshi hilo limeendelea kushirikiana na wadau wa usalama barabarani kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya barabara kupitia vyombo vya habari, shule za msingi, sekondari, vituo vya maegesho ya pikipiki na bajaji na vituo vya mabasi.

“Takwimu zinaonesha kuwa, matukio ya usalama barabarani yaliyotolewa taarifa katika vituo vya polisi nchini yamepungua kutoka 1,322 katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025 na kufikia 1,233 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2025/26.

Alisisitiza: “Katika matukio hayo, jumla ya watu 1,066 walipoteza maisha ikilinganishwa na watu 1,275 waliopoteza maisha katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2024/25 ikiwa ni upungufu wa asilimia 16.4. Vilevile, watu 1,869 walijeruhiwa ikilinganishwa na watu 2,278 waliojeruhiwa kwa kipindi kama hicho mwaka 2024/25 ikiwa ni upungufu wa asilimia 18.”

UNUNUZI VITENDEA KAZI

Waziri huyo alisema wamepokea sh. bilioni 247.4 kwa ajili ya ununuzi magari 412 na pikipiki 24 za kuongozea misafara. Alisema hadi Aprili mwaka huu, magari 76 na pikipiki 24 zimepokelewa huku magari 336 yanatarajiwa kupokelewa ifikapo Juni mwaka huu.

Aidha, alisema jeshi hilo limepokea sh. bilioni 64.79 ambazo zimetumika katika ununuzi wa vifaa vya kijeshi.

Alisema wizara kupitia jeshi hilo imenunua vifaa vya kisasa vya uchunguzi, mawasiliano pamoja na vifaa vya doria mtandaoni vyenye thamani ya sh. bilioni 182 kwa ajili ya kudhibiti uhalifu unaotokana na kukua kwa teknolojia.

“Upatikanaji vitendea kazi hivyo umeongeza ufanisi wa kazi kwa kufanya doria mtandaoni ili kuzuia matukio ya uhalifu na kuwezesha shughuli za upelelezi kufanyika kwa wakati,” alisisitiza.

WAFUNGWA WAMEPUNGUA MAGEREZANI

Katambi, alisema wizara yake kupitia Jeshi la Magereza imeendelea kudumisha hali ya ulinzi na usalama magerezani kwa kuimarisha operesheni za kiusalama pamoja na usimamizi wa magereza nchini.

Alisema katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili mwaka huu, wafungwa na mahabusu 23,514 walihifadhiwa na kupatiwa huduma za msingi ikiwemo chakula, malazi, mavazi na huduma za afya.
“Kati ya hao, wafungwa walikuwa 19,704 na mahabusu 3,810.

Takwimu hizo zinaonesha idadi ya wafungwa magerezani imepungua kwa asilimia 13.2 ikilinganishwa na idadi ya wafungwa na mahabusu 27,088 (wafungwa 19,400 na mahabusu 7,688) waliokuwepo magerezani katika kipindi kama hicho mwaka 2024/25.

MAONI YA KAMATI NA WABUNGE

Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Pascal Chinyele, alisema serikali iendelee kuongeza uwezo wa ndani katika fedha za maendeleo ili kupunguza utegemezi wa fedha za nje ambazo mtiririko wake siyo wa uhakika.

Pia, alisema kamati hiyo inashauri serikali iendeleze mikakati madhubuti na endelevu ya kuajiri watumishi wa kutosha kwa vyombo na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kukidhi mahitaji yaliyopo.

Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Makete (CCM), Festo Sanga, alipendekeza kuwepo mfumo wa lazima usajili wa wageni katika nyumba za kulala wageni na hoteli nchini kwa kutumia vitambulisho vya NIDA ili kuimarisha usalama wa nchi na kudhibiti na udanganyifu wa taarifa za wageni.

Alisema baadhi ya watu wamekuwa wakiingia katika maeneo ya malazi kwa kutumia majina ya uongo, jambo linaloweza kuhatarisha usalama na kuficha matukio ya kihalifu.

Alibainisha kuwa, matumizi ya NIDA kama kitambulisho cha msingi yatasaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya malazi na kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Katika bajeti hiyo, Bunge limeidhinisha sh. trilioni 2.4 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka 2026/27. Mchanganuo wa fedha hizo ni sh. trilioni 1.9 sawa na asilimia 80 ya bajeti yote ya wizara ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo, sh. trilioni 1.1 ni mishahara na sh. bilioni 769.5 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo huku sh. bilioni 489.8 sawa na asilimia 20 ya bajeti ni kwa miradi ya maendeleo.

Previous Post

KOCHA SIMBA ACHEFUKWA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WARIZI SANGU AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE MTAKA

WARIZI SANGU AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE MTAKA

2 months ago
HERI YA 2026, AMANI NDIYO MPANGO MZIMA

HERI YA 2026, AMANI NDIYO MPANGO MZIMA

5 months ago

Popular News

  • NEEMA YA AJIRA MAMBO YA NDANI

    NEEMA YA AJIRA MAMBO YA NDANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA ACHEFUKWA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SERENGETI BOYS AFUNGUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA YATAKA WAANDISHI KUHAMASISHA WAAJIRI KURIPOTI MATUKIO WCF

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?