• ePaper
Wednesday, September 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 27, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE
0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Dk. Mwigulu Nchemba amekutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo, Anatole Collinet Makosso na kujadiliana naye masuala ya kidiplomasia ikiwemo usalama, mazingira, kilimo na nishati kwenye kikao kilichofanyika ofisini kwa mwenyeji wake, Boulevard Alfred Raoul, Brazzaville, jijini Brazzaville.

Akizungumza na mwenyeji wake leo (Jumatano, Mei 27, 2026) Dk. Mwigulu amesema mbali na kupata fursa ya kushirki mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), ziara yake nchini Congo ni ya kukuza mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

“Ujio wetu nchini Congo Brazzaville, umelenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia lakini pia kuhimiza haja ya nchi zetu kukuza ushirikiano wa kikanda, kutunza utulivu, amani na maendeleo ya bara la Afrika.”

Alimwelezea mikakati ambayo Dkt. Samia ameiweka katika kukuza kilimo kupitia njia ya umwagiliaji, kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii na suala zima la uhifadhi wa mazingira.

Waziri Mkuu pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Congo, Denis Sassou-Nguesso kwa kumualika Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kushiriki mkutano huo ambao ilimpendeza kumtuma yeye amuwakilishe.

Ametumia fursa hiyo kufikisha ujumbe wa Dk. Samia wa kuiomba nchi ya Congo imuunge mkono mgombea wa Tanzania kwenye nafasi ya Jaji wa Mahakama ya Kimataifa (ICC), Dkt. Deo John Nangela ambaye uchaguzi wake umepangwa kufanyika Desemba, mwaka huu jijini New York, Marekani.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Congo alimshukuru Dk. Mwigulu kwa kushiriki mkutano huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alisema anatambua kwamba ana majukumu mengine ya kitaifa.

Alisema nchi hiyo ina mengi ya kujifunza kutoka Tanzania hasa kwenye sekta ya nishati. “Ninajua kwamba hakuna maendeleo bila uwepo wa umeme au nishati.

Na nchi ya Tanzania iliitisha mkutano mkubwa wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ujulikanao ‘misheni 300’ ambao unalenga kuhakikisha wananchi milioni 300 barani Afrika wanapata umeme ifikapo mwaka 2030. Tunapaswa tuungane kutafuta fedha za kuendeleza mradi huu,” alisisitiza.

Previous Post

MASTAA YANGA WAUTAJA UBINGWA LIGI KUU BARA

Next Post

‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

Next Post
‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WASIRA AONYA WANAOTOLEA MACHO UMEYA

WASIRA AONYA WANAOTOLEA MACHO UMEYA

12 months ago
MANNY PACQUIAO KUTUA BONGO NA MAMBO MAWILI

MANNY PACQUIAO KUTUA BONGO NA MAMBO MAWILI

8 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?