• ePaper
Wednesday, June 10, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA, SINGAPORE KUSHIRIKIANA KIMKAKATI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 10, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA, SINGAPORE KUSHIRIKIANA KIMKAKATI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SUPERIUS ERNEST

TANZANIA na Singapore, zimekubaliana kuendeleza na kuimarisha ushirikiano huku zikitia saini rasimu ya mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi (DTA).

Aidha, pande mbili hizo zimetaja maeneo ya kipaumbele ambayo ni biashara, uwekezaji, kuwapa vijana elimu ya ujuzi na mageuzi ya uchumi wa kidijitali.

Hayo yalibainishwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam, baada ya kushuhudia utiaji saini mikataba ya makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo.

Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, hati za makubaliana zilizokubaliwa na pande mbili hizo ni rasimu ya mkataba wa muondoa utozaji kodi mara mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi (DTA).

Hati hiyo ilitiwa saini na Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Omar kwa upande wa Tanzania na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Pili wa Wizara ya Fedha na Waziri wa Pili wa Maendeleo ya Kitaifa wa Jamhuri ya Singapore, Indranee Rajah.

Taarifa ya Kurugenzi hiyo ilisema lengo la hati hiyo ni kuchochea uwekezaji wa kigeni, kuongeza mauzo ya nje, kutoa uhakika wa kikodi kwa wawekezaji, kuimarisha ushirikiano wa kiutawala katika kuzuia ukwepaji wa kodi wa kimataifa kati ya mataifa hayo.

Ilisema hati nyingine iliyotiwa saini ni rasimu ya hati ya makubaliano kati ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ya Tanzania na Wizara ya Mambo ya Nje ya Singapore katika masuala ya uendelezaji ujuzi.

Hati hiyo ilitiwa saini na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete na Waziri wa Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje, Familia na Maendeleo ya Jamii wa

Singapore, Zhulkarnain Rahim.

Kwa mujibu wa taarifa, hati hiyo ina lengo la kuimarisha diplomasia ya uchumi, ushirikiano katika masuala ya uongozi na utawala, usalama wa chakula, usimamizi wa bandari, maji, huduma za anga na kuwajengea uwezo wataalamu katika masuala ya uongozi na utawala.

Nyingine iliyotiwa saini ni rasimu ya hati ya makubaliano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira wa Tanzania na Wizara ya Viwanda na Biashara ya Singapore katika biashara ya kaboni chini ya Ibara ya 6 ya Mkataba wa Paris.

Hati hiyo ilitiwa saini na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Hamad Yussuf Masauni na Waziri wa Nchi, Wizara ya Biashara na Viwanda na Wizara ya Maendeleo ya Kitaifa ya Singapore, Alvin Tan.

Pia, hati hiyo ina lengo la kuimarisha uhifadhi na usimamizi wa mazingira, kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani kuhusu biashara ya kaboni, kutoa elimu ya athari za hewa ukaa, kuandaa miradi ya nishati mbadala, kulinda bionuwai na uandaaji wa miradi chini ya Ibara ya 6 ya makubaliano ya Paris.

Rasimu ya hati ya makubaliano ya mashauriano ya uwili kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa 

Afrika Mashariki (Tanzania) na Wizara ya Mambo ya Nje ya Singapore, ilitiwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit

Kombo na Waziri wa Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje, Familia na Maendeleo ya Jamii wa Singapore, Rahim.

Hati hiyo ina lengo la kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Singapore.

Pande mbili hizo zitashirikiana katika masuala ya biashara na uwekezaji, utalii, uchumi wa buluu, uhandisi wa masuala ya bahari, kujengeana uwezo katika nyanja za mafunzo, mapinduzi ya kilimo chenye tija na fursa za ufadhili wa masomo.

Aidha, zitaimarisha uhusiano kwa kufanya vikao kila baada ya miaka miwili kuchambua hali ya utekelezaji wa maazimio yakiwemo maelekezo ya viongozi wa ngazi za juu na mikataba iliyotiwa saini. 

Ilieleza kuwa, rasimu ya hati ya makubaliano kati ya Wizara ya Viwanda na Biashara ya Tanzania na Taasisi ya Singapore Cooperation Enterprice (SCE) katika masuala ya uwezeshaji wa biashara, ilitiwa saini na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Kong Wy Mun.

Hati hiyo imelenga kushirikiana katika masuala ya viwanda na biashara nchini, hususani nyanja za maendeleo endelevu ya viwanda, ujenzi wa maeneo ya kibishara, maendeleo ya viwanda vidogo na vya kati (SME) na upatikanaji wa masoko.

Pia, uzalishaji wa viwandani, ushirikiano wa sekta binafsi katika uzalishaji wa viwanda na biashara, uvumbuzi na utafiti, mnyororo wa ugavi na uwekezaji biashara.

WALICHOSEMA MARAIS

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini makubaliano hayo, Rais Dk. Samia alisema lengo la ziara ya Rais Shanmugaratnam ni kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo.

“Ni heshima kubwa kwa nchi yetu kutembelewa na Rais wa Singapore, ni ziara ya kihistoria inayolenga kuimarisha ushirikiano wa mataifa yetu ikiwa imetimia miaka 45 ya ushirikiano huo muhimu wenye lengo la kukuza maendeleo ya nchi zetu na watu wetu,” alisema.

Alieleza kuwa, katika mazungumzo na Rais wa Singapore, walikubaliana kuendeleza ushirikiano huo, uwe imara na madhubuti utakaokuwa na matokeo yenye tija.

Alisema kwa kuanzia walitia saini mikataba mitano itakayoweka msingi wa kuendeleza ushirikiano huo.

“Matokeo mengine ya ushirikiano wetu ni masuala ya vijana, nimemweleza Rais kuwa, tumeanza utekelezaji wa Dira yetu ya Taifa ya Maendeleo na mwelekeo au kipaumbele kikubwa ni kuwaendeleza vijana ambao katika miaka 25 ijayo, ndiyo watakaokuwa wameshika nafasi maeneo mbalimbali,” alisema.

Alisema katika suala hilo la vijana, wamejipanga kuwawezesha kupata elimu yenye ujuzi, ukiwemo ujasiriamali na matumizi ya dijitali, ubunifu na kuwaimarisha katika mageuzi na utekelezaji uchumi wa kidijitali.

Rais Samia alisema hilo litatekelezwa katika miaka 10 na utekelezwaji huo, umeanza mwaka 2024 hadi 2034.

Dk. Samia alisema katika mikataba hiyo ya ushirikiano, wamelenga kushirikiana katika kilimo, kwa sababu Tanzania bado uchumi wake unategemea sekta hiyo.

Alieleza kuwa, wataimarisha suala hilo sawa na malengo ya mataifa hayo ya kuimarisha usalama wa chakula.

Aliwakaribisha wafanyabiashara wa Singaporea kuwekeza nchini katika sekta ya kilimo na kuzalisha nchini kama ambavyo walikubaliana na Russia, ambao wameanza uwekezaji na uzalishaji wa ndizi.

UIMARISHAJI BIASHARA

Rais Samia alisema uwekezaji wa nchi hizo una thamani ya dola za Marekani milioni 299 huku kukiwa na wawekezaji wa Singapore 36.

Alisema hali bado haiakisi tija ya ushirikiano huo, ndiyo maana wamekutana kujadili namna ya kufungua njia za kuukuza.

“Pia, tumegusia masuala ya biashara ya kikanda na Rais Shanmugaratnam, ameonesha nia ya kufanya mazungumzo katika jumuiya yetu ya Afrika Mashariki hususani eneo huru la biashara ikiwa sehemu ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi.

“Mimi na kwa niaba ya marais wenzangu, nimemkaribisha kwa mazungumzo hayo yenye tija,” alisema.

ATOA SHUKRANI

Dk. Samia alimshukuru Rais huyo wa Singapore kwa ziara yenye tija katika kukuza maendeleo ya wananchi na mataifa hayo mawili.

Pia, alieleza ushirikiano wa Tanzania na taifa hilo ni wenye tija.

Alimkaribisha Rais Shanmugaratnam kufungua ubalozi wa Singapore nchini.

SHANMUGARATNAM AFUNGUKA

Rais Shanmugaratnam akizungumza katika mkutano huo, alimshukuru Rais Samia kwa ukaribisho na mapokezi aliyopata akiwa na ujumbe wake.

Alisema kuwa, amefurahi kufika Tanzania kwa mara ya kwanza, ikiwa sehemu ya historia ya ushirikiano wa mataifa hayo yenye lengo la kuchochea ukuaji uchumi.

Alieleza Tanzania ni sehemu nzuri yenye vivutio vingi vya utalii na uwekezaji ukiwemo Mlima Kilimanjaro na sehemu zingine za utalii na uwekezaji zilizopo Zanzibar.

Alimhakikishia Rais Samia kuwa, nchi yake iko tayari kuimarisha ushirikiano huo kwa wananchi na maendeleo ya kiuchumi.

Shanmugaratnam alitaja maeneo waliyogusia katika mazungumzo hayo ni biashara na uwekezaji, kilimo, mageuzi ya kidijitali kwa vijana, diplomasia huku akitaja fursa nyingine iliyopo Tanzania ni eneo la uchumi wa buluu kupitia mlango wa Bahari ya Hindi.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA ANADI FURSA KEMKEMU

Next Post

YANGA, SIMBA VITA KALI

Next Post
YANGA, SIMBA VITA KALI

YANGA, SIMBA VITA KALI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KAULI UN YAWAKOSHA MABALOZI, WAHADHIRI

KAULI UN YAWAKOSHA MABALOZI, WAHADHIRI

6 months ago
MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

2 months ago

Popular News

  • YANGA, SIMBA VITA KALI

    YANGA, SIMBA VITA KALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA, SINGAPORE KUSHIRIKIANA KIMKAKATI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ANADI FURSA KEMKEMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WASOMI WADOKEZA MANUFAA YA UWEKEZAJI MAENEO MANNE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA ZATOA MSIMAMO LIGI KUU BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?