• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA, SIMBA MSHIKE MSHIKE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 22, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
YANGA, SIMBA MSHIKE MSHIKE
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WAKATI  Yanga ikimtambulisha Simo Dladla kuwa kocha msaidizi, klabu ya Simba imenasa saini ya mshambuliaji mzawa, Bakari Msimu kutoka klabu ya Coastal Union ya Tanga.

Taarifa zilizothibitishwa na  klabu zote mbili, Dladla atafanya kazi chini ya Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo, Manqoba Mngqithi kuhakikisha ubingwa wa Ligi Kuu Bara hauondoki mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.

Pia, Yanga imemtangaza kocha wa magolikipa, Greg Etafia kutoka Nigeria.

Yanga, imefanikiwa kumchukua Mtaalamu wa chambuzi wa Viwango na Mifumo ya Soka, Yardaan Valodia.

Hadi leo, Yanga imewasajili nyota wapya ambao ni Hussein Mihambo, Abdulnasir Mohamed wote kutoka Mashujaa FC ya Kigoma.

Yanga itakuwa na majukumu mengine ya kuhakikisha inafanya vizuri katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika(CAFCL) na Kombe la Shirikisho la CRDB lililoelekea Msimbazi msimu uliopita.

Lengo kuu la benchi hilo jipya la ufundi ni kuivusha Yanga kutoka hatua ya robo fainali waliyoizoea misimu ya hivi karibuni na kutinga hatua ya nusu fainali au fainali.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kuwa wana imani kubwa na kocha huyo kuwa atakuwa na msaada mkubwa katika kikosi chao.

Akizungumzia kuhusu kocha, Abdulhamid Moalin, Kamwe  alisema  bado ataendelea kusalia ndani ya kikosi hicho.

“Tumemtambulisha kocha mwenye CV kubwa kuwa msaidizi wa Mngqithi, hivyo tuna imani wataenda kushirikiana vyema ili kutimiza malengo tuliojiwekea msimu ujao,” alisema Kamwe.

Kwa upande wa Simba,Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally alisema kuwa wanaendelea kufanya usajili wa wachezaji wengi bora.

“Niwaambie tu mashabiki na wapenzi wa Simba kuwa tumesajili wachezaji wengi bora na wenye viwango hivyo wakae mkao wa kula kwani tutaendelea kushusha vifaa, kila siku,” alitamba.

Ahmed alisema Bakari Msimu amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi chao.

Tayari Simba imewasajili wachezaji wapya ambao ni Nathaniel Chilambo na Kelvin Nashon.

Wakati huo huo, Klabu ya Simba imemtangaza Emmanuel Nollo kama Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki.

Previous Post

KIGOMA KUMENOGA

Next Post

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA UWEKEZAJI AFYA AFRIKA

Next Post
RAIS DK. SAMIA AHIMIZA UWEKEZAJI AFYA AFRIKA

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA UWEKEZAJI AFYA AFRIKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AAHIDI MKAKATI WA NGANO

DK. SAMIA AAHIDI MKAKATI WA NGANO

10 months ago
DK. NCHIMBI : CCM ITAENDELEA KUMUENZI HAYATI KAWAWA

DK. NCHIMBI : CCM ITAENDELEA KUMUENZI HAYATI KAWAWA

10 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?