• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 23, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

IRENE MWASOMOLA NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza

WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde, amewabana wawekezaji wa nje wanaofanya ‘usanii’ wa kuwamilikisha hisa watu ambao siyo halisi wakiwemo madereva wa teksi katika kampuni zao za madini.

Pia, amewataka wasambazaji wazawa wanaotoa huduma hafifu migodini kutojificha katika kichaka cha uzawa.

Mavunde alisema hayo jijini Mwanza, alipofungua Jukwaa la Tano la Utekelezaji wa Ushirikishwaji Watanzania katika sekta ya madini.

Mavunde alisema amebaini baadhi ya wawekezaji, wametafuta madereva taksi na kuwasainisha hisa asilimia 20.

“Wale ambao mlitaka kuingia ubia, mmeingia nchini, ujanja umefanyika mkaenda kutafuta madereva teksi mkawasainisha (hisa) zile asilimia 20,”alisema.

Alisema tayari kuna kampuni moja serikali imeipa mwaka mmoja, imalizie muda wake iondoke nchini na kazi iliyokuwa inaifanya, itafanywa na Watanzania wenyewe.

Mavunde alisema lazima kila kampuni za uwekezaji, zifuate na kuheshimu sheria zilizotungwa nchini, licha ya kwamba wamekuja na mitaji.

“Hii ni nchi, lazima iheshimiwe, tutaendelea kutoa usaidizi kuhakikisha tunaboresha mazingira ya uwekezaji,”alisema.

Alisisitiza kuwa, hakuna mwekezaji wa kuipangia serikali na kujificha katika kichaka cha mitaji.

“Nimesikia wawekezaji mnasema mmekuja na mitaji, halafu mnapangiwa cha kufanya, nataka niwaambie mmekuja na mitaji madini mmeyakuta hapa Tanzania,”alisema 

Mavunde alisema anaamini mwekezaji anapokuja kuwekeza nchini anakuwa ameelewa sheria na taratibu .

Aidha Mavunde alisema baada ya kuwepo kwa changamoto hiyo serikali imefanya mabadiliko ya kanuni na kutibu.

Mavunde,  alisema wizara yake, imejizatiti kuona Watanzania wananufaika na asilimia 20 huku akiuagiza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kusaidia  kubaini  hilo.

TANZANIA YA TANO AFRIKA

Waziri huyo, alisema Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hivi sasa ina hifadhi tani 28 za dhahabu ambayo inaiwezesha kuingia miongoni mwa benki tano kati ya 10 zenye hifadhi kubwa ya madini hayo barani Afrika.

Alisema nchi inayoongoza kuwa na hifadhi ya madini kupitia benki kuu ni Algeria, ambayo ina tani 174 na ya mwisho ni Msumbiji ambayo ina tani 6.85

 “Ndani ya muda mchache leo Benki ya Tanzania ina hifadhi ya dhahabu tani 28 na kuingia tano bora ndani ya miezi 19, haya ni mafanikio chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,”alisema 

Kwa mujibu wa Mavunde, awali Tanzania haikuwepo katika nchi 10 bora ambazo zina uhifadhi mkubwa wa dhahabu kupitia benki kuu yake.

Mavunde, alisema mafanikio hayo yamefikiwa kutokana na marekebisho ya sheria, ambayo yameiwezesha BoT kuwa na hifadhi hizo.

Alisema mafanikio hayo, yalitokana na uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan, mwaka 2024 kuelekeza kufanya marekebisho ya sheria ya madini.

“Rais  Samia alitoa maelekezo mwaka 2024,  tukafanya marekebisho ya sheria kwa wakati ule kilikuwa kifungu cha 59,  kifungu kile kikafanyiwa marekebisho kikawa kinasomeka ifuatavyo, mmiliki yeyote wa leseni atatenga asilimia zisizopungua 20  za madini yanayozalishwa  kwa uchakataji, usafishwaji, uyeyushwaji na kufanyiwa biashara ndani  ya nchi.

“Hayo ndiyo marekebisho ya sheria, ambayo tuliyofanya, baada ya marekebisho hayo ya sheria, Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ilipata nafasi ya kuanza  kuwa mnunuzi wa dhahabu Oktoba Mosi 2024,  ilianza rasmi kununua dhahabu,”alisema.

Kuhusu mafanikio katika sekta ya madini nchini, Mavunde alisema sekta hiyo, imechangia mfuko wa maendeleo serikali zaidi ya sh. trilioni 1.3 hadi kufikia Juni 30, mwaka huu.

 Alisema kutokana na mapato hayo sekta hiyo imeongoza kwa mapato katika mapato yasiyo ya kikodi.

Pia, alisema Watanzania 16, 695 wameajiriwa katika ajira rasmi na wengine milioni 6 wakinufaika na sekta hiyo katika mnyororo wa thamani wa madini pamoja na fursa ya nafasi ya watendaji wakuu wa kampuni za migodi.

Akizungumzia ufunguzi wa migodi mipya ya madini, Mavunde alisema hadi hivi sasa serikali imeshaingia mikataba na kampuni 13 zitakazofungua shughuli za uchimbaji katika migodi.

Alisema ufunguzi wa migodi hiyo kutaongeza idadi ya migodi iliyopo hivi sasa, huku  akiwataka wasambazaji huduma kujiandaa.

“Migodi hiyo inakuja, kazi zinakuja mtachoka kazi je mko tayari, kajiungeni mfanye kazi fursa hii isiwatoke najua mna uwezo wa kufanya kazi,”alisema.

Katika ujenzi wa viwanda vinavyozalisha bidhaa zinazotumika katika migodi, Mavunde alisema serikali imepokea maombi ya kampuni 31 kutoka nje ya nchi kufungua viwanda hivyo.

 Waziri  Mavunde  alitoa rai kwa sekta binafsi kutumia fursa hiyo,  huku akisema katika maombi yaliyotolewa bado hakuna kampuni za wazawa zilizojitokeza.

Alisema serikali imetenga  eneo la Buzwagi mkoani Shinyanga,  kuwa eneo maalumu la viwanda vinavyozalisha bidhaa za migodini.  

Alisema  tayari wamepokea maombi yapatayo 31 kutoka kwa wawekezaji kutoka nje ya nchi.

MHANDISI YAHYA SAMAMBA

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Yahya Samamba, alisema serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya madini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

AMIR MKALIPA

 Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amir Mkalipa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, aliipongeza wizara kwa jitihada zake za kuendelea kuvutia uwekezaji mkoani humo.

Alisema uwekezaji huo umechangia kuanzishwa kwa Mgodi wa Dhahabu wa Sotta Mining, ambao unatarajiwa kutoa ajira 1,500 utakapoanza uzalishaji.

DK. JANET LEKASHINGO

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dk. Janet Lekashingo, alisema jukwaa hilo limekuwa na manufaa makubwa katika kuchochea ushiriki wa Watanzania katika sekta hiyo.

Alisema mafanikio hayo yanaonekana kupitia ongezeko la uwasilishaji wa mipango ya ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta hiyo kutoka mipango 51 mwaka 2018 hadi kufikia mipango 1,312 mwaka jana.

Previous Post

SERIKALI YATENGA BIL. 240/- KUJENGA MASOKO 30 NCHINI

Next Post

MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

Next Post
MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UWANJA WA BENJAMIN MKAPA WAFIKIA 90%

UWANJA WA BENJAMIN MKAPA WAFIKIA 90%

8 months ago
TUME YATAJA MAMBO 6  ITAKAYOYAFANYIA KAZI

TUME YATAJA MAMBO 6  ITAKAYOYAFANYIA KAZI

8 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?