• ePaper
Thursday, July 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

PPAA YAHIMIZA WAZABUNI KUTUMIA MODULI YA MALALAMIKO NA RUFAA KATIKA MFUMO WA NeST

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 30, 2026
in Habari, Kitaifa
0
PPAA YAHIMIZA WAZABUNI KUTUMIA MODULI YA MALALAMIKO NA RUFAA KATIKA MFUMO WA NeST
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Mwandishi Wetu, Arusha

MAMLAKA ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imewahimiza wazabuni na wadau wa ununuzi wa umma kutumia Moduli ya Kupokea na Kushughulikia Malalamiko na Rufaa katika mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) kuwasilisha malalamiko na rufaa zao PPAA pindi wanapoona hawakutendewa haki katika michakato ya ununuzi wa umma.

Akizungumza na waandishi wa Habari pembezoni mwa Kongamano la Kumi la ununuzi wa Umma la mwaka 2026 linaloendelea Jijini Arusha kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, James Sando, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma PPAA, Nelson Kessy amesema kuanza kwa matumizi ya Moduli hiyo kuna faida nyingi kama vile kuokoa muda na gharama.

“Faida nyingine za wazabuni na taasisi nunuzi kutumia moduli ni kuongeza uwazi na uwajibikaji, kuwezesha utunzaji kumbukumbu sahihi za malalamiko na rufaa zinazowasilishwa na wazabuni pamoja na kuongeza ufanisi katika utoaji wa uamuzi,” amesema Kessy

Kessy ameongeza kuwa Mamlaka ya Rufani inawaelekeza wazabuni wote wa ndani na nje ya nchi kutumia Moduli ya kuwasilisha Malalamiko na Rufaa kwa kuzingatia Sheria ya Ununuzi wa Umma pamoja na kanuni zake pindi wanapoona hawakutendewa haki katika zabuni walizoomba.

Katika hatua nyingine, Bw. Kessy amesema kuwa PPAA inatoa huduma ya Mkutano kwa njia ya Mtandao “Video Conference” ambapo hutumika kusikiliza mashauri ya wazabuni walioshindwa kufika moja kwa moja katika Ofisi za PPAA kwa ajili ya kusikiliza mashauri yalilowasilishwa mbele yake.

“Huduma ya Mkutano kwa njia ya Mtandao imetoa fursa ya kuwasikiliza wazabuni walioshindwa kufika PPAA kutokana na sababu mbalimbali na kuiwezesha Mamlaka ya Rufani kutekeleza jukumu lake la msingi la utatuzi wa migogoro itokanayo na michakato ya ununuzi wa Umma.

“Tangu kuanza kwa matumizi ya ‘video conference’ tayari PPAA imewasikiliza wazabuni mbalimbali kutoka katika mataifa ya Afrika Kusini, Nigeria, Poland, India na China,” amesema Kessy.

Kadhalika, amesema Mamlaka ya Rufani inatarajia kuunganisha Moduli ya Malalamiko na Rufaa na mfumo wa Mahakama ya Tanzania ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wakati na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma ikiwa ni njia mojawapo ya kuimarisha matumizi ya teknolojia katika sekta ya ununuzi wa umma.

Naye, mzabuni Peter Sarungi kutoka makundi maalumu alisisitiza sekta ya makundi maalumu ipewe kipaumbele zaidi katika uombaji wa zabuni na kufuatilia taasisi zilizotangaza zabuni ili wapewe taarifa kama wamepata zabuni au la ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi ikiwemo kutumia Moduli ya PPAA.

Matumizi rasmi ya moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST yalianza mwezi Februari, 2025.

Previous Post

SERIKALI KUANGALIA FURSA ZA MIKOPO KWA WANAOSOMA KOZI FUPI – WAZIRI MKUU

Next Post

SERIKALI KUZALISHA MAELFU YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

Next Post
SERIKALI KUZALISHA MAELFU YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

SERIKALI KUZALISHA MAELFU YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UWANJA WA SOKA DODOMA WAFIKIA 2.7%

UWANJA WA SOKA DODOMA WAFIKIA 2.7%

8 months ago
CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI

CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI

4 months ago

Popular News

  • SERIKALI KUZALISHA MAELFU YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

    SERIKALI KUZALISHA MAELFU YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PPAA YAHIMIZA WAZABUNI KUTUMIA MODULI YA MALALAMIKO NA RUFAA KATIKA MFUMO WA NeST

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUANGALIA FURSA ZA MIKOPO KWA WANAOSOMA KOZI FUPI – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALIYEOA MWANAFUNZI KWA MAHARI MILIONI 4/- ADAKWA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AGGREY MWANRI NAIBU KATIBU MKUU CCM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?