• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MWIGULU ADOKEZA FURSA YA AJIRA QATAR

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 30, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MWIGULU ADOKEZA FURSA YA AJIRA QATAR
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU, Doha, Qatar

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema Tanzania imepata fursa nyingine za ajira zaidi ya 4,500 kwa Watanzania walio tayari kufanya kazi Qatar kwa kada mbalimbali.

Amesema, alipotoa ufafanuzi kuhusu ziara yake ya siku tatu nchini Qatar na manufaa ambayo Tanzania imepata.

Dk. Mwigulu alikuwa nchini Qatar kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani.

“Tunatarajia kupata nafasi nyingine 4,500 kwa Watanzania ambazo ziko katika hatua za mwisho za kukamilisha utaratibu.

“Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, ndiyo inaratibu zoezi zima kwa kushirikiana na wizara za kisekta, ikiwemo ya Mambo ya Ndani pamoja ile ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,” alisema Dk. Mwigulu.

Tanzania imekuwa ikinufaika na fursa za ajira nchini Qatar, ambapo hadi hivi sasa, kuna Watanzania 720 walioajiriwa katika Kampuni ya Taifa ya Usafirishaji ya Qatar (MOWASALAT) ikiwa ni sehemu ya nafasi za ajira 2,000 zilizotolewa katika awamu ya kwanza.

Katika awamu ya pili, Kampuni ya Power Holding International, imetoa nafasi za ajira zaidi ya 4,000 kwa Watanzania wenye ujuzi mbalimbali.

Akielezea kuhusu mazungumzo yao, Dk. Mwigulu alisema walijadili kuhusu hati mbili za makubaliano ambazo zilitiwa saini juzi na waliafikiana kwamba, hati moja iliyobaki ya kuepusha ukwepaji kodi na utozaji wa kodi mara mbili, ikamilishwe itiwe saini mapema iwezekanavyo.

Hati zilizotiwa saini ni ya Makubaliano ya Ushirikiano katika maeneo ya Zimamoto, Uokoaji na Huduma za Dharura kati ya  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Taifa la Qatar na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. ,

Nyingine ni Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa Kisiasa na Kidiplomasia baina ya Taifa la Qatar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Ziara hii kimsingi ililenga kutilia mkazo maeneo yaliyokubaliwa na viongozi wetu wakuu wa nchi wakati walipokutana,” alisema.

Dk. Mwigulu, alitumia fursa hiyo kumwalika Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Al Thani, afanye ziara nchini Tanzania, kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kufuatilia utekelezaji wa mambo waliyokubaliana.

Alisema kuwa, katika ziara yake, alikutana na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika mwaka 2022 nchini Qatar.

“Lengo lilikuwa ni kupata uzoefu wao katika kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa na yakafanikiwa kwa kiwango cha juu sana.

“Hii ni fursa kwetu kwa sababu Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoandaa michuano ya Kombe la Mataifa Huru ya Afrika hapo mwaka kesho,” alisema.

Katika ziara hiyo, Dk. Mwigulu alifuatana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ngwaru Maghembe, Katibu Wakuu (OR-Uwekezaji), wabunge na watendaji wengine wa serikali.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA ATEUA MA-DC 22

Next Post

SHAKA : DK. SAMIA AMEWAHESHIMISHA WANAWAKE AFRIKA

Next Post
SHAKA : DK. SAMIA AMEWAHESHIMISHA WANAWAKE AFRIKA

SHAKA : DK. SAMIA AMEWAHESHIMISHA WANAWAKE AFRIKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UMUHIMU KUNYWA MAJI HUU HAPA

UMUHIMU KUNYWA MAJI HUU HAPA

6 months ago
AHMED ALLY AJIVUNIA GUEYE

AHMED ALLY AJIVUNIA GUEYE

7 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?