• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SHAKA : DK. SAMIA AMEWAHESHIMISHA WANAWAKE AFRIKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 30, 2026
in Habari, Kitaifa
0
SHAKA : DK. SAMIA AMEWAHESHIMISHA WANAWAKE AFRIKA
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, amesema kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imewaheshimisha wanawake wa Tanzania na kuwa Kielelezo kwa bara zima la Afrika.

Shaka aliyasema hayo wakati akitoa salamu katika uzinduzi wa Wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Dumila, uliofanyika katika mji wa Dumila, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

“Alama aliyoiacha Dk. Samia kwa Watanzania si ujenzi wa madaraja na barabara tu, alama yake kubwa ni kutuonyesha kwamba Mtanzania hana kikomo. Leo ukitaka kujua mafanikio ya mwanamke yanaonekanaje, haangalii tena Ulaya, anaangalia Ikulu ya Tanzania,” alisema Shaka ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa na kushangiliwa na mamia ya wanawake waliohudhuria uzinduzi huo.

Aidha, Shaka amesema Wiki ya UWT sio sherehe tu bali ni kipimo cha kutathmini heshima ya mwanamke katika jamii.

“Wiki ya UWT ni kutathmini heshima ya mwanamke. Rais Samia ametufundisha kuwa heshima ya mwanamke si zawadi, ni haki.

“Kielelezo hakifi bali kinadumu. Heshima ya Dk. Samia iliyoandikwa kwa wino wa dhahabu itaendelea kuwa urithi wa kizazi kwa kizazi. Wino wa dhahabu haufutiki mvua ikinyesha wala jua likiwaka,” amesisitiza.

Katika sherehe hizo, mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda, aliyeambatana na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya umoja huo.

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mbunge wa Kilosa ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Profesa Palamagamba Kabudi.

Previous Post

MWIGULU ADOKEZA FURSA YA AJIRA QATAR

Next Post

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UMMA KATIKA MKUTANO WA IPU

Next Post
RAIS DK. SAMIA AHIMIZA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UMMA KATIKA MKUTANO WA IPU

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UMMA KATIKA MKUTANO WA IPU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MTIFUANO MKALI NNE BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

MTIFUANO MKALI NNE BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

5 months ago
WAZIRI KOMBO NA PROF. KABUDI WAITEMBELEA KAMBI YA TAIFA STARS

WAZIRI KOMBO NA PROF. KABUDI WAITEMBELEA KAMBI YA TAIFA STARS

10 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?