• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. MWINYI KUSHUSHA RUNGU WATENDAJI GOIGOI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 23, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa
0
RAIS DK. MWINYI KUSHUSHA RUNGU WATENDAJI GOIGOI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi

0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na HANIFA RAMADHANI,
Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema, hatomvumilia mtendaji yeyote ambaye atashindwa kwenda katika maeneo yenye matatizo na kusubiri kuletewa taarifa ofisini.

Amewaasa watendaji, kuacha kukaa ofisini, badala yake, kwenda kwa wananchi kutatua changamoto zinazowakabili. 

Dk. Mwinyi, aliyasema hayo baada ya kuwaapisha makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu, hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja.

Alisema serikali yake haitomvumilia mtendaji anayeshindwa kwenda katika maeneo yenye matatizo, kwani imezoeleka mara nyingi watu wamekuwa wakikaa ofisini na kusubiri mafaili bila ya kutoka nje.

Aidha, alisema utaratibu wa kusubiri mafaili ofisini, umepitwa na wakati, uongozi wa sasa, unahitaji watumishi wenye kasi, ubunifu na utayari wa kuwasikiliza wananchi.

“Kuna tabia ya watu kukaa ofisini wakisubiri mafaili waletewe, huo si utendaji tunaoutaka katika awamu hii, tunahitaji viongozi wanaotembea, wanaofuatilia na wanaotatua changamoto kwenye maeneo husika,” alisisitiza.

Dk. Mwinyi, alibainisha kuwa, ipo mifano ya matatizo madogo, lakini yanachukua muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi kutokana na watendaji kukaa ofisini.

“Nadhani itoshe sasa kwani wananchi wa nchi hii, wana matarajio makubwa na sisi, mimi nitakuwa mmoja katika kuhakikisha yoyote yule ambae hatekelezi majukumu yake, basi anatupisha kwani lengo letu ni kuona yale tuliyoyaahidi yanatimia,” alisema.

Aliwasisitiza watendaji kutumia nafasi walizopewa kuboresha utoaji huduma za umma pamoja na kuongeza uwajibikaji katika taasisi zao.

Aliahidi kufanya kikao kazi na watendaji wote aliowateua na wale wa zamani, wakiwemo mawaziri kuzungumzia matarajio yake katika utekelezaji wa shughuli za serikali wanapoanza awamu hiyo mpya ya pili ya utendaji wake.

AWAPA VITENDEA KAZI VITANO

Sambamba na hayo, Dk. Mwinyi alivitaja vitendea kazi vikuu vitano kwa awamu ya pili ya Serikali ya Awamu ya Nane, ambavyo ni pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2025/2030.

Alisema lazima kila mtu angalie sekta yake, inaekezwa nini katika ilani na kupanga mpango kazi wa kuhakikisha kwamba, inatekelezwa kwa asilimia100.

Jambo la pili, alisema ni kuisoma hotuba aliyoitoa Baraza la 11 la Wawakilishi, kwani kuna maeneo mengi ambayo amezungumza, yote yanataka utekelezaji, kwani ni ahadi alizoitoa.

Dk. Mwinyi, alisema ahadi alizozitoa kipindi cha kampeni kwa wananchi na ofisi yake itatoa orodha ya aliyoahidi na kila taasisi na wizara, kuangalia maono yake kwa madhumuni ya kujipanga na kutekeleza kwa muda mfupi.

Alibainisha kwamba, wakijipanga vizuri katika utekelezaji wa maeneo hayo, hana shaka wataweza kukidhi matakwa ya wananchi ambayo waliyasema kipindi cha kampeni.

“Kwangu, mimi zile ni ahadi na muungwana akiahidi anatekeleza, hivyo, ninyi ndiyo watendaji na mnatambua majukumu yenu katika wizara na maofisa masuuli katika wizara zenu,” alisema.

AKEMEA MAKUNDI

Dk. Mwinyi alikemea suala la makundi ndani ya wizara, kwani uwepo wake, hautaweza kutekeleza majukumu kwa ufanisi.

Hivyo, aliwataka kuhakikisha wanayaondoa makundi hayo na kushirikiana kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi.

“Niwatake kama watawala katika wizara, hakikisheni mnaondoa makundi, watu wote wanakua wamoja na mnafanya kazi ya wananchi waliotukabidhi,” aliwasisitiza.

Rais Mwinyi, aliwasisitiza ukusanyaji wa mapato katika wizara zao na kuzingatia matumizi vyema, kwani bado kuna changamoto ya ukusanyaji hafifu wa mapato na kuwepo kwa matumizi makubwa ambayo hayana sababu za msingi.

Alisema hayo yote hayatawezekana bila ya kuwa na rasilimali fedha, hivyo lazima kama ofisa masuuli kuyasimamia hayo.

Aliwapongeza wote waliopokea uteuzi wake na kuwatakia kazi njema na majukumu mema na kutekeleza yale ambayo wameahidi wananchi.

Walioapishwa ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Fatma Mabrouk Khamis, Katibu Mkuu,  Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Khamis Suleiman Mwalim, Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Dk. Habiba Hassan Omar, Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango Dk. Rahma Salim Mahfoudh na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji Salama Mbarouk Khatib.

Wengine walioapishwa ni Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Saleh Mohamed Juma, Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo,Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Ali Said Bakar.

Pia, aliwaapisha naibu makatibu wakuu ambao ni Rashid Ali Salum Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Uwezeshaji, Makame Machano Haji Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo,Khalid Masoud Waziri Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji, Dk. Mohammed Dhamir Kombo Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo na Amos John Henock Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (Utawala).

Previous Post

AMANI NGUZO KUU YA USTAWI – RAIS DK. SAMIA

Next Post

SERIKALI YATOA TAMKO

Next Post
SERIKALI YATOA TAMKO

SERIKALI YATOA TAMKO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DAKTARI ATAJA DALILI ZA SHINIKIZO LA DAMU

DAKTARI ATAJA DALILI ZA SHINIKIZO LA DAMU

1 month ago
CCM YAELEZA KUONGEZEKA MBOLEA YA RUZUKU

CCM YAELEZA KUONGEZEKA MBOLEA YA RUZUKU

9 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?