• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA MGENI RASMI MKUTANO IPU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 5, 2025
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA MGENI RASMI MKUTANO IPU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan

0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Arusha
NA LILIAN JOEL 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaotarajiwa kufanyika mwakani jijini Arusha ambao utahudhuriwa na wageni zaidi ya 1500 kutoka mataifa mbalimbali.

Hayo yalibainishwa jijini hapa, baada ya ujumbe wa IPU ukiongozwa na Balozi Ande Filip ulipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano huo.

Balozi Ande alisema mkutano huo utahudhuriwa maspika, wabunge na viongozi zaidi ya 1500 kutoka mataifa mbalimbali duniani ambapo Rais Dk. Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

“Kulingana na ratiba, washiriki tutakuwa hapa kwa zaidi ya siku sita ambapo baada ya kumalizika kwa mkutano, watapata fursa kutembelea  maeneo ya kihistoria na vivutio vya utalii vilivyopo Mkoa wa Arusha,” alieleza.

Awali, akiukaribisha ujumbe huo, Makalla alisema Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa sababu ya ushiriki na historia yake katika Bunge la  IPU.

“Sisi tumewahakikishia tupo tayari kuwa wenyeji wa mkutano huo, tupo tayari kuwapa ushirikiano kufanikisha mkutano huo mkubwa wa kihistoria.

“Tanzania ni Mwenyeji kwa sababu ya ushiriki wake wa historia katika IPU. Kikubwa zaidi ni namna wao wanavyoiona Tanzania, sisi tumewahakikishia tupo tayari kuwapa ushirikiano kufanikisha mkutano huo mkubwa,” alieleza.

Alisisitiza: “Hii ni fursa kwetu kwa Tanzania kuendelea kuaminika kimataifa. Niwaombe  wananchi kujiandaa kutumia fursa za ujio wa mkutano huo kiuchumi.”

Previous Post

VIJANA LINDENI AMANI YA NCHI – DK. MIGIRO

Next Post

WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA KUANZA MASOMO KWA MKUPUO

Next Post
WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA KUANZA MASOMO KWA MKUPUO

WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA KUANZA MASOMO KWA MKUPUO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WAZIRI CHONGOLO AELEKEZA MIFUMO TOSCI ISOMANE

WAZIRI CHONGOLO AELEKEZA MIFUMO TOSCI ISOMANE

5 months ago
WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIDAIWA KUIBA MALI ZA SH. BILIONI 1.5

WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIDAIWA KUIBA MALI ZA SH. BILIONI 1.5

4 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?