• ePaper
Monday, June 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

BONDIA MWAKYEMBE KUTOA ZAWADI YA KRISMASI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 11, 2025
in Burudani, Michezo
0
BONDIA MWAKYEMBE KUTOA ZAWADI YA KRISMASI

Emmanuel Mwaykembe

0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

BONDIA wa ngumi za kulipwa, Emmanuel Mwaykembe amehaidi kutoa zawadi ya sikukuu ya Krisimasi katika pambano lake la Punch To Punch’ litakalofanyika Jumapili ya wiki  hii.

Mwakyembe atapanda ulingoni kuzichapa na Tionge Chingeni kutoka Malawi katika pambano lisilo la ubingwa raundi nane, uzito wa kati litakalofanyika Ukumbi wa The Sea View Dome Banguel ulipo Kawe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam, jana,bondia huyo alisema hivi sasa anafanya mazoezi mepesi huku akisubiri kupima uzito, keshokutwa katika Viwanja vya Las Vega Mabibo.

“Niko fiti kabisa nahitaji kutoa zawadi ya sikukuu ya Krisimasi kwa Watanzania wote na mashabiki zangu kwa ujumla,” alisema.

Mwakyembe aliongeza kuwa Watanzania wanapaswa kufurahia mafanikio ya mchezo wa ngumi na yeye atawapa.

“Hivi sasa Tanzania inafanya vizuri katika michezo mbalimbali ndiyo maana sisi mabondia tunapambana kuongeza bidii katika mazoezi, kuwapiga wapinzani wetu kutoka nje ya nchi kama kwangu nipo fiti na pambano langu kumchakaza Mmalawi,” alisema Mwakyembe.

Promota wa pambano hilo, Latifa Jabiri alisema mpinzani wa bondia Mwakyembe, ameshafika Tanzania anasubiri siku ya kupima uzito.

“Kila kitu kinaenda vizuri kutakuwa na mapambano makali nina imani wadau wa masumbwi watafurahi kwa sababu kila bondia atayepanda ulingoni ataonyesha mchezo nzuri na kutoa burudani ya kutosha,” alisema.

Promota huyo alisema kutakuwa na mapambano 15 ambayo wadau wa masumbwi watashuhudia vijana wakipimana ubavu.

Previous Post

MASTAA YANGA, SIMBA WAPEWA PROGRAMU ZA MAZOEZI

Next Post

WATAALAMU WATAJA MAMBO 8 KUEPUKA UHABA WA MAJI DAR

Next Post
WATAALAMU WATAJA MAMBO 8 KUEPUKA UHABA WA MAJI DAR

WATAALAMU WATAJA MAMBO 8 KUEPUKA UHABA WA MAJI DAR

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

2 months ago
IDADI WAGONJWA FIGO YAFIKIA 3,342

IDADI WAGONJWA FIGO YAFIKIA 3,342

3 months ago

Popular News

  • YANGA, SIMBA ZATOA MSIMAMO LIGI KUU BARA

    YANGA, SIMBA ZATOA MSIMAMO LIGI KUU BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWANZA KINARA USIMAMIZI MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WFP KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA USIMAMIZI WA MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HESHIMA KUBWA KWA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU: MAMBO MAZURI YANAKUJA, AIPA TANO SERENGETI BOYS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?