• ePaper
Sunday, May 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

NADO, MASAGALA WATOA NENO STARS

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 13, 2025
in Burudani, Michezo
0
NADO, MASAGALA WATOA NENO STARS

WACHEZAJI STARS

0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WACHEZAJI wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Idd Seleman ‘Nado’ na Hussein Masalanga wamesema wapo tayari kupambana kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wachezaji wa timu hiyo, walisema wapo tayari kwa ajili ya vita ya kusaka taji hilo na kuwapa furaha Watanzania.

Idd Selemani ‘Nado’, alisema kuwa kwanza ni furaha kwake kushiriki AFCON kwa mara ya kwanza na atahakikisha anapambana ili kufunga mabao katika mashindano hayo.

Alifafanua kuwa kila mchezaji ana shauku kubwa ya kuipambania timu yao na jinsi wanavyoendelea kupata mafunzo kutoka kwa Kocha Miguel Gamondi.

“Kwanza niseme, kambi yetu ni nzuri na mwalimu amekuwa akitupa mbinu tofauti tofauti kuhakikisha tunashinda katika kila mchezo, kwa upande wangu kitu kinachotakiwa ni kuifungia timu yangu mabao, naamini hii itakua nafasi nzuri ya kuonesha kipaji changu,” alisema Nado.

Mchezaji huyo alisema kuwa timu yao inaendelea kufanya mazoezi kwa bidii, wachezaji wote wako katika ari kubwa ya kushindana na kuipatia heshima Tanzania.

Kipa wa timu hiyo, Hussein Masalanga alisema wachezaji wote wanafanya mazoezi kwa bidii, kujiandaa ipasavyo na mashindano hayo yatakayofanyika nchini Morocco.

Masagala alisema kwa upande wa makipa wanaendelea kujipanga ili kuwa bora na kutoruhusu mabao katika mashindano hayo.

“Mashindano haya ni makubwa kwa Afrika, hivyo sisi wachezaji hatutakubali kuwa wanyonge, tunaendelea kufanya maandalizi ya kutosha ili tuwe katika kiwango bora na kutimiza malengo tuliyojiwekea,” alisema Masagala.

Hii ni mara ya nne, Stars kufuzu fainali za AFCON ikishiriki mara ya kwanza mwaka 1980 nchini Nigeria, mwaka 2019 michuano iliyofanyika nchini Misri na mwaka 2023 ilichezwa nchini Ivory Coast.

Previous Post

TFF. BMT WANOGESHA SAFARI MASHABIKI AFCON

Next Post

JESS NAZ APATA MAJANGA

Next Post
JESS NAZ APATA MAJANGA

JESS NAZ APATA MAJANGA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WANANCHI KUSINI UNGUJA WAAHIDI KUIPIGIA KURA CCM

WANANCHI KUSINI UNGUJA WAAHIDI KUIPIGIA KURA CCM

8 months ago

Uchumi wa Tanzania unaendelea kukua kwa asilimia 6.8

9 months ago

Popular News

  • DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

    DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU MOGAE WA BOTSWANA, AKIMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA NI NCHI YA PILI AFRIKA KUWA NA HADHI YA  UTALII WA JIOLOJIA (GEOPARK MUSEUM)

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAIPONGEZA PUMA ENERGY KWA MFUMO MPYA WA KIDIJITALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?