• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

IDADI WAGONJWA FIGO YAFIKIA 3,342

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 11, 2026
in Habari, Kitaifa
0
IDADI WAGONJWA FIGO YAFIKIA 3,342
0
SHARES
18
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SIMON NYALOBI

WAKATI leo Tanzania inaungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Figo Duniani, wagonjwa 3,342 wanaendelea kupatiwa huduma ya uchujaji damu nchini.

Hayo yalisemwa na Mratibu wa Huduma za Figo wa Wizara ya Afya, Dk. Abdi Chaula, alipozungumza na gazeti hili kuhusu ugonjwa wa figo.

Kwa mujibu wa Dk.  Chaula kumekuwa na ongezeko la wagonjwa hao kutoka wagonjwa 1,017 waliokuwepo mwaka 2019 hadi kufikia 3,342 mwaka huu.

“Hali ya ugonjwa ilivyo hivi sasa kuna wagonjwa 3,342 wa figo wanaopatiwa huduma ya uchujaji wa damu katika vituo 73 vinavyotoa huduma hiyo kote nchini,”alisema.

Aidha, wagonjwa 177 walipandikizwa figo kupitia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) katika matawi yake ya Upanga na Mloganzila jijini Dar es Salaam na Hospitali ya Benjamin Mkapa ya jijini Dodoma.

Akizungumzia sababu za ongezeko la wagonjwa  wa figo nchini, alisema kumetokana na sababu mbalimbali, zikiwemo mabadiliko ya mtindo wa maisha ya watu katika nyanja za ulaji na matumizi ya pombe kupita kiasi.

Dk. Chaula alizitaja sababu nyingine ni kutofanya mazoezi, matumizi makubwa ya chumvi, kutokunywa maji ya kutosha na kutokuwa na utamaduni wa kupima afya kila wakati.

Alifafanua ugonjwa huo hauna tabia ya kuonesha dalili za awali, hali inayosababisha watu wengi kwenda hospitali wakiwa katika hatua za mwisho ya kuathirika.

“Hatuna utamaduni wa kupima afya kila wakati na ugonjwa huo katika hatua za mwanzo hauna dalili hadi hatua ya tano ndiyo huonesha dalili,  ambayo tayari ugonjwa unakuwa umefikia pabaya,”alisema.

Alishauri jamii kujenga tabia ya kupima afya angalau mara moja kwa mwaka, hali itakayowasaidia kugundua iwapo wana ugonjwa huo mapema.

Kuhusu jitihada za serikali kukabiliana na ugonjwa huo, alisema serikali imejikita katika kutoa elimu kwa jamii katika kubadilisha mtindo wa maisha kupitia vyombo vya habari.

Alieleza serikali imetoa mwongozo wa mtindo bora wa maisha na mwongozo wa kufanya mazoezi kuepukana na ugonjwa huo.

Aidha,  alisema imeongeza wigo wa tiba kuongeza vituo vya tiba ambapo alisema vituo vya tiba vimeongezeka kutoka 17 vilivyokuwa mwaka 2017 hadi 73.

Kwa mujibu wa Chaula, serikali imepunguza gharama matibabu ya uchujaji damu kwa mzunguko mmoja kutoka sh. 250,000 hadi sh. 150,000.

Previous Post

DK. MWIGULU AWAVAA WANAOSUBIRI UTEUZI

Next Post

UN YAIFAGILIA TANZANIA KWA AMANI

Next Post
UN YAIFAGILIA TANZANIA KWA AMANI

UN YAIFAGILIA TANZANIA KWA AMANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA : UTAKUWA UCHAGUZI WA AMANI

DK. SAMIA : UTAKUWA UCHAGUZI WA AMANI

8 months ago
MGOMBEA Mwenza wa Urais, Dk. Emmanuel Nchimbi, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Butiama, mkoani Mara. (Picha na Abdurahman Jumanne)

BALOZI DK. NCHIMBI AZURU KABURI LA HAYATI MWALIMU NYERERE

9 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?