• ePaper
Sunday, April 5, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SERIKALI YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NISHATI ZA DOLA BIL. 12.9

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 20, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
SERIKALI YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NISHATI ZA DOLA BIL. 12.9
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Tanzania imetangaza uwepo wa fursa kubwa za uwekezaji katika sekta ya nishati zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 12.9, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukuza uchumi na kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati nchini.

Akizungumza katika mjadala kuhusu ushirikiani wa Marekani na Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa Powering Africa Summit leo Machi 20, 2026 jijini Washington DC, Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema uwekezaji huo unahitajika katika maeneo mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa umeme, usafirishaji, usambazaji pamoja na nishati safi ya kupikia.

Ameeleza kuwa katika sekta ya uzalishaji wa umeme, miradi 13 imepangwa kutekelezwa ndani ya miaka mitano ijayo, ikihitaji uwekezaji wa dola bilioni 2.77, hatua itakayowezesha kuongeza megawati 1,421 za umeme nchini.

Kwa upande wa miundombinu ya usafirishaji wa umeme, amesema jumla ya miradi 23 yenye thamani ya dola bilioni 1.21 inapangwa kujengwa, ikiwemo kilomita 1,350 za njia za kusafirisha umeme pamoja na vituo vya kupozea umeme.

Aidha, Salome amebainisha kuwa kuna fursa nyingi katika sekta ya gesi asilia, akieleza kuwa Tanzania ina zaidi ya futi za ujazo trilioni 57 za gesi ambazo bado hazijatumika kikamilifu.

Amesisitiza umuhimu wa uwekezaji katika uchimbaji, usindikaji na matumizi ya gesi hiyo katika uzalishaji wa umeme na shughuli za viwandani.

Katika hatua nyingine, amesema Serikali inaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, ikilenga kufikia asilimia 75 ya matumizi hayo ifikapo mwaka 2030. Mpango huo unahusisha usambazaji wa majiko bora, gesi pamoja na teknolojia nyingine rafiki kwa mazingira.

Salome amewahimiza wawekezaji walioshiriki mkutano huo kutumia fursa zilizopo kuwekeza nchini, huku Serikali ikiendelea kuboresha mazingira ya biashara na kuweka sera rafiki kwa uwekezaji.

Katika Mkutano huo Naibu Waziri Salome ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Else Sia Kanza na wataalam kutoka Wizarani, TANESCO, REA pamoja na PURA.

Previous Post

WARIZI SANGU AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE MTAKA

Next Post

TUSHEREHEKEE EID KWA UTULIVU, AMANI

Next Post
TUSHEREHEKEE EID KWA UTULIVU, AMANI

TUSHEREHEKEE EID KWA UTULIVU, AMANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MADAKTARI BINGWA WAFUNGUKA MBINU KUKABILI ‘PRESHA’

MADAKTARI BINGWA WAFUNGUKA MBINU KUKABILI ‘PRESHA’

3 months ago
TANZANIA MFANO BORA SEKTA YA MAJI DUNIANI

TANZANIA MFANO BORA SEKTA YA MAJI DUNIANI

2 weeks ago

Popular News

  • CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI

    CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MCHENGERWA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AELEZA FAIDA YA KULINDA TUNU YA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VIONGOZI WA DINI WAHUBIRI AMANI 

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?