• ePaper
Sunday, April 5, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. MWINYI: MEMA YA MFUNGO WA RAMADHANI YAENDELEZWE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 21, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK. MWINYI: MEMA YA MFUNGO WA RAMADHANI YAENDELEZWE
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewasisitiza waumini wa dini ya Kiislamu kuyaendeleza mambo mazuri waliyokuwa wakiyatekeleza mwezi wa Ramadhani.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo alipojumuika na waumini wa dini ya kiislamu katika swala ya Ijumaa iliyofanyika Msikiti wa Maisara mjini Unguja.

Alisema Ramadhani ni kipindi cha kujifunza mema na kumalizika kwake, haipaswi kuwa sababu ya kurudi katika maovu, bali ni fursa ya kuendeleza maadili mema na kuzidi kumcha Mungu.

KIFO CHA IMAM

Katika hatua nyingine, Rais Mwinyi aliwapa pole waumini wa msikiti huo kufuatia kifo cha Imam wao, Sheikh Saleh Ameir kilichotokea juzi.

Pia, alitumia fursa hiyo kuwatakia wananchi wote heri na furaha katika kusherehekea sikukuu ya Eid el Fitri leo.

MAKAMU WA PILI WA RAIS

Wakati huohuo, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Hemed Suleiman Abdulla, aliwataka wazazi na walezi kuhimizana kuwadhibiti watoto hasa kipindi cha sikukuu hiyo ya Eid.

Abdulla alisema hayo jana alipowasalimia waumini wa Masjid ya Rahmaan uliopo Mfenesini, Wilaya ya Magharibi “A“ baada ya swala ya Ijumaa.

Alisema kuwadhibiti watoto katika sikukuu ni jambo la lazima kwa kila mzazi kuwakinga na majanga ikiwemo udhalilishaji.

“Suala la ulinzi kwa watoto huanza na mzazi na kuwasisisiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto sehemu ambazo ni salama,” alisisitiza.

Abdulla alisema wazazi wanapaswa kuwavalisha watoto nguo za heshima kuwajenga katika maadili mema pamoja na kuwakinga na vishawishi mbalimbali wakiwa katika matembezi.

Mbali na hilo, aliwasisitiza waumini wa dini ya kiislamu na Wazanzibari kwa ujumla, kuendelea kuiombea nchi pamoja na viongozi wakuu walete maendeleo na kuipigania amani na utulivu.

Previous Post

TUSHEREHEKEE EID KWA UTULIVU, AMANI

Next Post

MWANASHERIA WA KWANZA MWANAMKE UDSM AFARIKI

Next Post
MWANASHERIA WA KWANZA MWANAMKE UDSM AFARIKI

MWANASHERIA WA KWANZA MWANAMKE UDSM AFARIKI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DEPU, OKELLO WAMOTO, YANGA IKISHINDA 6-0

DEPU, OKELLO WAMOTO, YANGA IKISHINDA 6-0

3 months ago
KISHINDO CHA DK. NCHIMBI RUVUMA

KISHINDO CHA DK. NCHIMBI RUVUMA

7 months ago

Popular News

  • CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI

    CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MCHENGERWA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AELEZA FAIDA YA KULINDA TUNU YA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VIONGOZI WA DINI WAHUBIRI AMANI 

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?