• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. KIKWETE ATEULIWA KUWA MWAKILISHI WA NGAZI YA JUU WA MWENYEKITI WA KAMISHENI YA AU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 25, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
DK. KIKWETE ATEULIWA KUWA MWAKILISHI WA NGAZI YA JUU WA MWENYEKITI WA KAMISHENI YA AU
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Mahmoud Ali Youssouf, amemteua Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Mwenyekiti wa AUC katika eneo la Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu.

Uteuzi huo umetangazwa rasmi leo, Machi 25, 2026, unalenga kuimarisha juhudi za Umoja wa Afrika katika kushughulikia changamoto za kisiasa, amani, na masuala ya kiusalama yanayoikabili kanda hiyo.

Kufuatia uteuzi huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amempongeza Dk. Kikwete na kueleza kuwa ni heshima kubwa kwake na kwa Tanzania. Aidha, amemtakia majukumu mema katika kuimarisha Umoja wa Afrika na kupata suluhu ya amani ya kudumu kwa manufaa ya Afrika na ulimwengu wote.

Katika nafasi hiyo, Dk. Kikwete atakuwa na jukumu la kuunga mkono jitihada za AU kupitia: kuendeleza diplomasia ya kuzuia migogoro na kuratibu mazungumzo jumuishi ya kisiasa. Aidha, kujenga uaminifu miongoni mwa wadau mbalimbali wa kikanda na kuimarisha ushirikiano wa kikanda unaolenga kukuza amani na utulivu wa kudumu.

Dk. Kikwete, kama Mwakilishi wa Ngazi ya Juu, atafanya kazi kwa uratibu wa karibu na AU na washirika muhimu wa kikanda na kimataifa, ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo (IGAD), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Umoja wa Nchi za Kiarabu, na Umoja wa Mataifa (UN) ili kujenga amani na utulivu wa kudumu.

Ushirikiano huo ni muhimu kutokana na nafasi ya kimkakati ya Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu kwa biashara ya kimataifa na utulivu wa Bara la Afrika kwa ujumla.

Youssouf ameeleza kuwa na imani kubwa na uzoefu, uongozi, na hekima za Dkt. Kikwete, na kwamba atatoa mchango mkubwa katika kuzisaidia nchi za kanda hiyo kukabiliana na changamoto zilizopo, kukuza ustawi pamoja na amani ya kudumu.

Uteuzi huu unakuja wakati ambapo eneo la Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu linaendelea kuhitaji ushirikiano wa karibu wa kidiplomasia ili kuhakikisha usalama wa kanda na ulinzi wa njia kuu za biashara duniani.

Previous Post

MAKONDA : TUMEJIPANGA KUTWAA AFCON 2027

Next Post

MATARAJIO YA WASOMI TUME YA JAJI CHANDE

Next Post
MATARAJIO YA WASOMI TUME YA JAJI CHANDE

MATARAJIO YA WASOMI TUME YA JAJI CHANDE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIMBU APANDISHWA CHEO

SIMBU APANDISHWA CHEO

8 months ago
AZAM KUSAKA MAKALI KUIVAA SIMBA

AZAM KUSAKA MAKALI KUIVAA SIMBA

2 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?