• ePaper
Saturday, June 6, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. JAKAYA AKUTANA NA RAIS RUTO JIJINI NAIROBI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 17, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
DK. JAKAYA AKUTANA NA RAIS RUTO JIJINI NAIROBI
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU 

RAIS Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwenye Eneo la Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Kenya, William Ruto.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao walipata fursa ya kuzungumzia mchakato wa kutafuta amani nchini Sudani Kusini, hususan kwa kuzingatia nafasi ya Kenya katika mgogoro wa nchini huo.

Moja ya jitihada za kuleta amani nchini Sudani kusini zimefanywa na Serikali ya Kenya kupitia Mpango wa Amani wa Tumaini ambao umelenga kuvijumuisha katika mazungumzo ya amani vikundi vyote vya kijamii na vya kijeshi ambavyo havikutia saini katika Makubaliano ya Amani nchini Sudani Kusini R-ARCSS yaliyosainiwa Mwaka 2018.

Ziara hiyo ya Rais Mstaafu Dk. Kikwete ni sehemu ya kutekeleza kujumu lake jipya la kuwa mpatanishi wa amani nchini Sudani Kusini, ambapo tangu kuteuliwa kwake ameweza kukutana na Viongozi mbalimbali wenye ufuasi katika hali ya amani, ulinzi na usalama nchini Sudani kusini wakiwemo Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na sasa Rais William Ruto wa Kenya.

Aidha, Dk. Kikwete ameshafanya ziara nchini Sudani Kusini na kukutana na Makundi yote muhimu katika mgogoro huo kwa lengo la kukubaliana mkakati endelevu utakaohakikisha amani inarejea katika nchi hiyo changa kuliko zote barani Afrika

Previous Post

RAIS DK. SAMIA ATOA MWELEKEO WA KITAIFA

Next Post

USALAMA MZURI KUWALETA NCHINI WABUNGE 2000 IPU

Next Post
USALAMA MZURI KUWALETA NCHINI WABUNGE 2000 IPU

USALAMA MZURI KUWALETA NCHINI WABUNGE 2000 IPU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KOCHA SIMBA KICHEKO  

KOCHA SIMBA KICHEKO  

3 weeks ago
SH. TRILIONI 3.5 ZIMETOLEWA KUWEZESHA VIJANA – MAJALIWA

SH. TRILIONI 3.5 ZIMETOLEWA KUWEZESHA VIJANA – MAJALIWA

8 months ago

Popular News

  • MWANZA KINARA USIMAMIZI MAAFA

    MWANZA KINARA USIMAMIZI MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WFP KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA USIMAMIZI WA MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HESHIMA KUBWA KWA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU: MAMBO MAZURI YANAKUJA, AIPA TANO SERENGETI BOYS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERENGETI BOYS HESHIMA KILA KONA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?