• ePaper
Thursday, May 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SIMBA, COASTAL HAPATOSHI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 21, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
SIMBA, COASTAL HAPATOSHI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

TIMU za soka za Simba na Coastal Union zinatarajiwa kupambana leo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Pambano hilo, limepangwa kufanyika leo katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kuanzia saa 12:30 jioni.

Kuelekea mchezo huo, kocha wa Simba, Steve Barker alisema kila mchezo kwao ni kama fainali, hivyo wamejipanga kupata alama tatu muhimu.

“Unajua tunaelekea mwishoni mwa msimu, hatukubali kuona tunapoteza mchezo wowote ule kwani ushindi ni muhimu.

“Tunamuheshimu mpinzani na tunaingia katika mchezo wetu kuonyesha kiwango kizuri, kulingana na maandalizi mazuri yaliofanyika kwa wachezaji wangu, naamini tunakwenda kupata ushindi katika mchezo huu,” alisema Barker.

Kocha huyo alisema amefanyia kazi kasoro zote zilizojitokeza katika michezo iliyopita.

Nyota wa timu hiyo, David Kameta alisema kama wachezaji wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo muhimu.

 “Baada ya mchezo uliopita wachezaji wote tumefanya maandalizi mazuri na kila mmoja yupo tayari kuhakikisha tunapambana kusaka pointi tatu,” alisema Kameta.

Kocha wa Coastal Union Fikiri Elias, alisema timu yake imejipanga vizuri kuhakikisha inashinda mchezo huo, wakiwa uwanja wao wa nyumbani.

“Hatutaki kuwa daraja la kumnyanyua yoyote lazima tutafute alama tatu kwa ajili ya timu yetu na kujiweka nafasi nzuri zaidi,” alisema Elias.

Kocha huyo alisema kila mchezo una ladha yake na wamejiandaa vizuri kucheza dakika 90 kwa kumpa heshima mpinzani wao.

Nahodha wa timu hiyo, Geofrey Manyasi alisema kama wachezaji wamejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda pambano hilo.

Katika msimamo wa Ligi, Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 52 huku Coastal Union ikishika nafasi ya 11, ina alama 25 baada ya timu zote mbili kushuka dimbani mara 23.

Previous Post

RIO USIPIME KABISA

Next Post

KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

Next Post
KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WIZARA YA VIWANDA YAZALISHA AJIRA LUKUKI NDANI YA SIKU 100

WIZARA YA VIWANDA YAZALISHA AJIRA LUKUKI NDANI YA SIKU 100

3 months ago
TUUNGANE KUJENGA NCHI – BALOZI NYALANDU

TUUNGANE KUJENGA NCHI – BALOZI NYALANDU

4 weeks ago

Popular News

  • KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, COASTAL HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIO USIPIME KABISA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA KICHEKO  

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?