• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KILOSA YAANZA MAANDALIZI YA KUKABILIANA NA EL NINO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 24, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KILOSA YAANZA MAANDALIZI YA KUKABILIANA NA EL NINO
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MKUU wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka ameongoza Kikao Maalum cha Kamati ya Maafa ya Wilaya kilichojumuisha Kamati ya Ulinzi na Usalama na wadau mbalimbali kujadili maandalizi ya kukabiliana na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Akifungua kikao hicho, Shaka amesema Wilaya ya Kilosa imejifunza kutokana na athari za mafuriko ya miaka ya nyuma na safari hii maandalizi yote yatajikita kwenye vitendo, sio kwenye makaratasi.

Amefafanua kuwa uamuzi huo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyeagiza mikoa na wilaya zote kuchukua tahadhari mapema na kuhakikisha taarifa za TMA hazibaki kwenye makaratasi bali zinafuatwa na hatua za vitendo.

Akizungumza kwa msisitizo, DC Shaka alisema:

“Wilaya ya Kilosa tumeamua fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya maafa zitanunua vifaa vya dharura vinavyoonekana. Sitaki kusikia mafunzo, semina na warsha.

Wananchi wa Kilosa wanajua mafuriko ni nini. Wanachohitaji ni boti la kuwaokoa, blanketi la kujifunika na dawa wakiumwa.”

“Nimesikia kuna fedha zimetengwa kwa ajili ya mafunzo ya maafa. Sitaki kusikia mafunzo.

Sitaki kabisa. Nani hapa Kilosa hajui mafuriko? Mtoto wa miaka 10 wa Kimamba anajua mafuriko kuliko mtaalamu. Fedha zozote za maafa zisiguse mafunzo.”

“Mafuriko yakija kesho, hutamwambia mama aliyekwama na watoto wawili juu ya paa – ‘Mama subiri nikupe brochure ya mafunzo’. Hapana. Utamwambia – ‘Mama panda boti, hiki hapa blanketi, huu hapa mchele’.”

Kwa upande wao, wadau mbalimbali walioshiriki kikao hicho wamepongeza utaratibu wa Wilaya ya Kilosa wa kushirikisha makundi yote na kueleza kuwa mipango iliyopangwa itatekelezeka na kuhakikisha usalama wa wananchi katika kipindi hiki cha tahadhari.

Kikao kimeazimia kuanzishwa kwa Stoo ya Dharura ya Wilaya na kuhamishwa kwa wananchi wanaoishi maeneo hatarishi.

Previous Post

KWAHERI BIBI FATUMA KARUME, DAIMA TUTAKUKUMBUKA

Next Post

LATRA YAFICHUA SIRI YA MAFANIKIO YAKE

Next Post
LATRA YAFICHUA SIRI YA MAFANIKIO YAKE

LATRA YAFICHUA SIRI YA MAFANIKIO YAKE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

PAWASA, MTEMI WAZIPA MCHONGO YANGA, SIMBA

PAWASA, MTEMI WAZIPA MCHONGO YANGA, SIMBA

9 months ago
SITAWAANGUSHA

SITAWAANGUSHA

6 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?