• ePaper
Sunday, November 16, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Burudani

YANGA, SIMBA ZAANZA KUCHONGA 

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 7, 2025
in Burudani, Kitaifa, Michezo
0
YANGA, SIMBA ZAANZA KUCHONGA 
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WAKATI timu za Simba na Yanga zikitarajiwa kurejea kuwapa burudani mashabiki na wapenzi wa soka nchini katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, viongozi wa timu hiyo wametamba kuwa watajizolea pointi tatu muhimu.

Simba inatarajiwa kushuka dimbani kesho kupambana na timu ya JKT Tanzania katika mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo, kuanzia saa 1:00 usiku.

Kwa upande wa Yanga, itashuka dimbani kupambana na KMC, siku ya Jumapili katika pambano litakalopigwa Uwanja wa KMC, kuaniza saa 10:00 jioni.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alitamba kuwa timu yao imejipanga vizuri kuelekea katika mchezo huo.

“Tunaifahamu vizuri timu ya JKT Tanzania, wana kikosi bora na chenye ushindani mkubwa, lakini hatutakubali kupoteza mchezo huo,”alisema meneja huyo.

Ahmed alisema kuwa hawatakubali kuona wanadondosha pointi yeyote katika mechi zao za mzunguko wa kwanza kwani lengo kubwa ni kutimiza malengo waliojiwekea.

“Tunaingia katika mchezo mgumu na wenye changamoto kubwa, kwani JKT Tanzania inawachezaji wengi wenye ubora hivyo watahakikisha wanapambana kuweza kupata ushindi na kujizolea pointi tatu muhimu,” alisema Ahmed.

Ahmed aliwaomba mashabiki na wapenzi wa soka nchini kufika kwa wingi uwanjani ili kuwapa hamasa  wachezaji wao washinde pambano hilo.

Naye Ofisa Habari wa Yanga Ally Kamwe alitamba kuwa wanaenda katika mchezo wao dhidi ya KMC kwa tahadhari kubwa  ili kupata ushindi.

Alisema kwa sasa kila timu imejipanga kuhakikisha inashinda mechi zake za ndani na nje ili kupata pointi tatu muhimu.

“Kila mchezo kwetu ni fainali, tumejipanga vizuri kushinda kwani malengo yetu ni kupata ushindi,” alisema.

Kamwe alifafanua kwamba mashabiki na wapenzi wa soka nchini wanatakiwa kufika uwanjani kwa wingi uwanjani ili kushuhudia soka ya kiwango cha juu kutoka kwa wachezaji wa Yanga.

Mechi zingine ni Pamba Jiji dhidi ya Singid Black Stars utakaochezwa Novemba 8, mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Namungo itacheza Novemba 9, mwaka huu na timu ya Azam FC,pambano litakalopigwa Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.

Previous Post

GAMONDI AMPA MAJUKUMU KELVIN JOHN

Next Post

AZAM YAZITOLEA MACHO WYDAD, NAIROBI UTD NA AS MANIEMA

Next Post
AZAM YAZITOLEA MACHO WYDAD, NAIROBI UTD NA AS MANIEMA

AZAM YAZITOLEA MACHO WYDAD, NAIROBI UTD NA AS MANIEMA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI

DK. SAMIA KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI

1 month ago
TRA YAHAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO USALAMA

TRA YAHAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO USALAMA

18 hours ago

Popular News

  • YANGA, SIMBA KAZI KAZI

    YANGA, SIMBA KAZI KAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KETE YA KWANZA KWA GAMONDI STARS LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TRA YAHAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO USALAMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAAGIZO MATATU KWA DK. NCHEMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NI MARIDHIANO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.