• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MATOLA AWAFUNGIA KAZI WASHAMBULIAJI SIMBA SC

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 6, 2025
in Burudani, Michezo
0
MATOLA AWAFUNGIA KAZI WASHAMBULIAJI SIMBA SC

KAIMU Kocha Mkuu wa Simba, Selemani Matola

0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ABDUL DUNIA

PAMOJA na kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Selemani Matola, amesema bado ana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha washambuliaji wake wanatumia vyema nafasi zinazotengenezwa.

Simba ilipata ushindi huo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Katika mtanange huo ambao Mbeya City ilimaliza pungufu kwa straika wake Vitalis Mayanga kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 28, Simba ilikosa nafasi nyingi za wazi.

Kuhusu ukosaji wa nafasi za wazi, Matola alikiri huku akisema kwamba, ana kazi kubwa ya kufanya kwa nyota wake kuhakikisha wanakuwa makini katika eneo la mwisho.

“Ninafikiri ni tatizo letu kubwa kutumia nafasi, tuna kazi kubwa sana ya kubadilisha nafasi kuwa magoli,” alisema.

Hata hivyo, Matola aliipongeza timu yake kwa ushindi huo huku akisema ni jambo zuri kwenda kuchuana na Azam FC kesho wakiwa wametoka kupata ushindi.

“Ni kitu kizuri, imetupa nguvu kubwa kuelekea katika dabi ya Mzizima, haitakuwa mechi rahisi lakini ni jambo zuri kupata ushindi tukielekea katika dabi,” alisema.

Simba itachuana na Azam FC kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Katika michuano hiyo, Simba ipo nafasi ya tano kwa alama 12 katika mechi nne, ikifunga mabao 11 na kuruhusu moja huku Azam FC ikiwa nafasi ya 12 kwa alama sita katika mechi nne, ikifunga mabao manne na kuruhusu mawili.

Previous Post

TWIGA STARS YAPEWA MCHONGO WAFCON

Next Post

KIHONGOSI: TANZANIA HAIWEZI KURUDI UKOLONI

Next Post
KIHONGOSI: TANZANIA HAIWEZI KURUDI UKOLONI

KIHONGOSI: TANZANIA HAIWEZI KURUDI UKOLONI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TASWIRA VIGOGO VINNE LIGI KUU BARA IKO HIVI

TASWIRA VIGOGO VINNE LIGI KUU BARA IKO HIVI

3 months ago
GAMONDI ALIA NA MUUNGANIKO

GAMONDI ALIA NA MUUNGANIKO

9 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?