• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RC MTAKA AWAPA SOMO LA AMANI VIJANA WA NJOMBE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 8, 2025
in Habari, Kitaifa
0
RC MTAKA AWAPA SOMO LA AMANI VIJANA WA NJOMBE

MKUU wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka

0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ELIZABETH JOHN

MKUU wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, amesisitiza umuhimu wa vijana na wananchi kuendelea kulinda amani kuwa ndiyo msingi wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mtaka alisema hayo katika Ibada ya Kanisa la Waadventista Wasabato, Njombe Mjini alipokuwa akizungumza na waumini ambapo alieleza kwamba vijana wa kizazi kipya wana nafasi kubwa katika kulinda na kuimarisha misingi ya taifa.

“Vijana wetu wa Gen-Z wana wajibu wa kulinda amani ya Tanzania, hiki ndiyo kizazi kinachobeba matumaini na sura ya taifa letu,” alisema.

Mtaka alisisitiza hakuna taifa linaloweza kusonga mbele bila haki na uwajibikaji, huku akisisitiza amani ya Tanzania imekuwa matokeo ya jitihada za wananchi kutimiza wajibu wao kwa umoja.

“Amani ni tunda la haki na wajibu, ni msingi thabiti wa maendeleo yetu. Tunao wajibu wa kuilinda amani ya nchi yetu kwa wivu mkubwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo,” aliongeza.

Katika eneo la usalama wa mkoa, Mtaka alisema Njombe inabaki kuwa miongoni mwa maeneo salama nchini na haina matishio ya uhalifu.

Alifafanua kuwa serikali ya mkoa inaendelea kuimarisha mifumo ya ulinzi wa watu na mali zao kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao za uzalishaji bila hofu.

“Usalama wa mkoa wetu utatuongezea imani kwa wawekezaji kuendelea kuona Njombe kama sehemu sahihi ya kuweka mitaji yao,” alisema huku akiwataka wananchi kuungana kuzuia tafrani zinazoweza kuharibu mali au miradi ya maendeleo.

Aidha, Mtaka aliwasihi wananchi kujenga tabia ya kutoa taarifa mapema mara wanapotilia shaka hali inayoweza kuhatarisha amani katika maeneo yao, kwamba ulinzi shirikishi hauwezi kusimama bila ushiriki wa wananchi.

Previous Post

LATRA YAONGEZA VIBALI 70 MABASI MIKOANI

Next Post

TULIENI NYUMBANI

Next Post
TULIENI NYUMBANI

TULIENI NYUMBANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KOCHA SIMBA AGEUKIA LIGI KUU

KOCHA SIMBA AGEUKIA LIGI KUU

4 months ago
PM MWIGULU ASISITIZA USHIRIKIANO VIONGOZI WA DINI, SERIKALI 

PM MWIGULU ASISITIZA USHIRIKIANO VIONGOZI WA DINI, SERIKALI 

6 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?