• ePaper
Wednesday, April 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. NCHIMBI ATOA AGIZO KWA PROF. MKENDA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 16, 2025
in Habari, Kitaifa
0
DK. NCHIMBI ATOA AGIZO KWA PROF. MKENDA

MAKAMU wa Rais Balozi, Dk.Emmanuel Nchimbi

0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ANGELA SEBASTIAN,
Bukoba

MAKAMU wa Rais Balozi, Dk.Emmanuel Nchimbi, amemwagiza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, kutatua changamoto ya fedha za ujenzi wa bweni la wavulana na nyumba za walimu kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tawi la Kagera.

Balozi Dk. Nchimbi, alieleza hayo mjini hapa, alipoweka jiwe la msingi la ujenzi unaoendelea wa majengo ya tawi la chuo hicho katika vijiji vya Itahwa na Kangabusharo wilayani Bukoba.

Alisema ujenzi huo uliopo chini ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET), unatekelekelezwa mikoa yote nchi nzima.

Alisema lengo ni kuwezesha idadi kubwa ya vijana wanapata elimu yenye ubora na ujuzi wa kuwakwamua kiuchumi.

“Ujenzi wa chuo hiki ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kukuza uchumi na kuchochea maendeleo ya Mkoa wa Kagera na taifa, lengo ni kuhakikisha kila mkoa unapata tawi la chuo kikuu,”alisema Balozi Dk. Nchimbi.

Aidha, Balozi Dk. Nchimbi, aliagiza uongozi wa chuo hicho, kuhakikisha mitaala inayotolewa inaendana na utolewaji elimu ya amali ya kuwawezesha wanafunzi kujiajiri baada  ya kuhitimu.

Makamu wa Rais, alisema serikali itatekeleza maombi ya ujenzi wa mindombinu ya barabara zinazozunguka chuo hicho kwa kiwango cha lami ili kukipa hadhi chuo.

Naye Mkuu wa Chuo, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, alisema chuo hicho, kitachochea kwa kiwango kikubwa ukuaji wa uchumi kwa wananchi wa Kagera.

Kikwete, alisema Rais Samia amejibu ombi la wananchi wa Kagera kutaka mkoa huo kuwa na chuo kikuu cha kuendelea kuzalisha wasomi wengi.

Aliwataka viongozi wa Kagera, kuongeza ukubwa wa eneo jingine nje ya lililopo, kwa ujenzi endelevu kwa sababu, mkakati ni kuhakikisha tawi hilo linakuwa Chuo Kikuu kinachojitegemea.

Previous Post

KAULI UN YAWAKOSHA MABALOZI, WAHADHIRI

Next Post

AWESO AAGIZA MGAWO MAJI UWE SHIRIKISHI

Next Post
AWESO AAGIZA MGAWO MAJI UWE SHIRIKISHI

AWESO AAGIZA MGAWO MAJI UWE SHIRIKISHI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

YANGA, MBEYA CITY KAZI IPO LEO

YANGA, MBEYA CITY KAZI IPO LEO

6 days ago
SAFARI KUMALIZA CHANGAMOTO UMEME IRINGA, DODOMA YAIVA

SAFARI KUMALIZA CHANGAMOTO UMEME IRINGA, DODOMA YAIVA

3 months ago

Popular News

  • YANGA YATIMUA VUMBI CAF, SIMBA MMH

    YANGA YATIMUA VUMBI CAF, SIMBA MMH

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AMPA TANO SIMBU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?