• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAGAMBO AAHIDI KUENDELEZA MAFANIKIO YA PSSSF

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 17, 2025
in Habari, Kitaifa
0
MAGAMBO AAHIDI KUENDELEZA MAFANIKIO YA PSSSF
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI mteule wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Fortunatus Magambo, ameahidi kuendeleza mafanikio yote yaliyoanzishwa na mtangulizi wake kwa maslahi mapana ya Taifa, wanachama na wananchi kwa ujumla.

Magambo ameyasema hayo Desemba 16, 2025, wakati wa hafla ya kukabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Dk. Rhimo Nyansaho, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Magambo amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini na kumteua kuiongoza PSSSF na kuwapongeza watangulizi wake kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kuimarisha Mfuko huo.

“Kwa kushirikiana na wenzangu, nitahakikisha tunaendeleza kazi nzuri zilizofanyika, kwa lengo la kuhakikisha wanachama wetu, hususan wastaafu, wanapata huduma sahihi na kwa wakati,” amesema Magambo.

Kwa upande wake, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Dk. Nyansaho, aliwataka watumishi wa Mfuko huo kuendelea kutendeana mema, akisema hatua hiyo itaongeza morali ya kazi na kuchangia utoaji wa huduma bora kwa wanachama.

Dk. Nyansaho pia aliishauri menejimenti ya PSSSF kuwekeza katika miradi yenye tija kwa Mfuko na Taifa kwa ujumla, hususan miradi inayozalisha ajira kwa vijana na kutoa soko kwa bidhaa zinazozalishwa na Watanzania.

Aidha, ameitaka menejimenti kuhakikisha watumishi wanaendelea kufanya kazi katika mazingira salama na yenye furaha, akiwashukuru kwa ushirikiano waliompatia kipindi chote cha uongozi wake.

Dk. Nyansaho ameteuliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Mbunge na baadaye kuteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Previous Post

NAIBU WAZIRI MAGHEMBE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA DHARURA WA SADC

Next Post

WAZIRI KOMBO NA PROF. KABUDI WAITEMBELEA KAMBI YA TAIFA STARS

Next Post
WAZIRI KOMBO NA PROF. KABUDI WAITEMBELEA KAMBI YA TAIFA STARS

WAZIRI KOMBO NA PROF. KABUDI WAITEMBELEA KAMBI YA TAIFA STARS

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI : DK. SAMIA KIONGOZI WA MAJAWABU

DK. NCHIMBI : DK. SAMIA KIONGOZI WA MAJAWABU

8 months ago
SPIKA ZUNGU : NITAZINGATIA HAKI, UWAZI

SPIKA ZUNGU : NITAZINGATIA HAKI, UWAZI

7 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?