• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MAJIHA APANIA KUTETEA MKANDA WBO AFRIKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 30, 2025
in Burudani, Kitaifa, Michezo
0
MAJIHA APANIA KUTETEA MKANDA WBO AFRIKA
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA 

BONDIA wa ngumi za kulipwa, Mtanzania Fadhili Majiha, amesema anaendelea kujipanga vyema kuutetea mkanda wake wa ubingwa WBO Afrika.

Majiha atapanda ulingoni kutetea mkanda huo Januari 31 mwaka huu, jijini Dar es Salaam, ambapo hadi sasa bondia atakayechapana naye hajajulikana.

Akizungumza Dar es Salaam, Majiha alisema mashabiki na wadau wa ngumi nchini wategemee burudani bora kutoka kwake.

Alisema muda umefika wa yeye kutetea mkanda huo wenye thamani kubwa.

“Ninahitaji sapoti kutoka kwa wadau wa ngumi kwani Januari 31, mwakani, ninatarajia kutetea mkanda wa ubingwa WBO Afrika, muda umefika wa kuonyesha kazi nzuri kwa Watanzania.

“Mpinzani atawekwa wazi ni bondia mwenye viwango kutokana na aina ya mkanda ambao tunacheza, najua Watanzania na mashabiki zangu wanatambua uwezo wangu na kazi ambayo mara nyingi nimekuwa nikifanya bila ya kuwaangusha, “alisema Majiha.

Bondia huyo alisema hivi sasa anafanya mazoezi ya kujiandaa na pambano hilo kwani malengo yake ni kuendelea kumiliki mkanda huo, ndiyo maana anapambana kujiweka fiti.

Kocha wa bondia huyo, Kwame Khamisi, alisema burudani nzuri inakuja hivyo ni muhimu kumuombea dua Majiha afanye kazi yenye kiwango kikubwa.

Alisema mara nyingi Majiha anakutana na mabondia wagumu ambao Afrika wamekuwa tishio,lakini yeye anawapiga na kupata ushindi bila tatizo.

Previous Post

SIMBA QUEENS MENO NJE, YANGA YALIA NA WACHEZAJI

Next Post

EL KAABI ANAWIRI AFCON

Next Post
EL KAABI ANAWIRI AFCON

EL KAABI ANAWIRI AFCON

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AAHIDI NEEMA ZAIDI GAIRO

DK. SAMIA AAHIDI NEEMA ZAIDI GAIRO

11 months ago
MATOLA AWAFUNGIA KAZI WASHAMBULIAJI SIMBA SC

MATOLA AWAFUNGIA KAZI WASHAMBULIAJI SIMBA SC

8 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?