• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WASOMI WADOKEZA CHANZO WANAFUNZI KUANDIKA MATUSI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 12, 2026
in Habari, Kitaifa, RIPOTI MAALUMU
0
WASOMI WADOKEZA CHANZO WANAFUNZI KUANDIKA MATUSI
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ELIZABETH JOHN

WASOMI wameeleza kuwa, tukio la baadhi ya wanafunzi kuandika lugha isiyofaa ‘matusi’ katika mitihani ya taifa ni ishara ya wazi ya mmomonyoko wa maadili unaoanzia ngazi ya malezi na makuzi ya watoto nyumbani.

Pia, wameshauri kuwepo kwa hatua za kinidhamu zitakazotumika kama funzo kwa wengine, huku wakisisitiza kuwa adhabu hizo zieleweke kama malezi, si ukatili.

Akizungumza na UHURU, Mhadhiri wa Idara ya Uongozi, Maadili na Utawala wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dk. Philip Daninga, alisema chanzo kikubwa cha tabia hiyo ni kukosekana kwa misingi ya maadili tangu utotoni.

Alisema maadili au tabia njema, hujengwa kwanza nyumbani, kisha kuimarishwa shuleni na katika jamii kwa ujumla, ni vigumu mtoto anayelelewa katika mazingira yenye maadili mema kufika kwenye chumba cha mtihani na kuamua kuandika matusi badala ya kujibu maswali.

“Ukiona mtoto anafanya hivyo, ujue kuna mahali pamelegea, maadili yanaanzia nyumbani. Shule na maeneo mengine, yanakuja kuyakuza,” alisema.

Dk. Daninga, aliwataka wazazi kutimiza wajibu wao wa msingi wa kulea na kuwaongoza watoto katika maadili mema, huku akiwapongeza walimu kwa mchango wao mkubwa kwa malezi ya watoto shuleni.

 “Badala ya kutupiana lawama, tufanye mambo ya kijamii kwa pamoja. Mtoto anapoandika matusi katika mtihani, hilo ni suala la maadili na uadilifu,” aliongeza.

Aidha, alishauri kuwepo kwa hatua za kinidhamu zitakazotumika kama funzo kwa wengine, huku akisisitiza kuwa adhabu hizo zieleweke kama malezi, si ukatili.

Alisisitiza kuwa, misingi ya maadili inasisitiza kumrekebisha mtoto mapema kabla tabia haijakomaa.

“Mtoto wa darasa la nne kufikia hatua hiyo, ni tabia iliyoanza mapema, kuanzia darasa la pili au la tatu. Ndiyo maana ni muhimu kuchukua hatua mapema na kuelimisha wale ambao bado hawajafika katika hatua hiyo, kumtandika viboko mtoto ni moja ya mafunzo,” alisema.

Mchumi na mtafiti mwandamizi, Profesa Samwel Wangwe, alieleza kuwa, pamoja na malezi, sababu nyingine zinazopaswa kuchunguzwa ni mazingira ya ujifunzaji, ikiwemo ukubwa wa madarasa na uwezo wa wanafunzi kuelewa maswali.

 Alisema kuandika matusi kunaashiria kuwa mwanafunzi ana uwezo wa kuandika, lakini huenda anakosa uelewa wa kujibu maswali au anachagua kufanya hivyo kutokana na malezi duni.

“Sina uelewa sana na hili kwa sababu sijawahi kufundisha shule ya msingi, lakini kabla ya kuchukua hatua, wanapaswa kuchunguzwa mazingira wanayotoka na waulizwe nini kimewasukuma kufanya hivyo,” alisema.

WANASAIKOLOJIA

Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasaikolojia Tanzania (TAPA), Albano Michael, alisema hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja kwa sababu hali hiyo inabebwa na mambo mengi hasa ukiangalia huwa haijulikani anayetukanwa nani.

“Mtoto anayefika hatua ya kutumia lugha chafu katika mazingira rasmi kama chumba cha mtihani mara nyingi huwa amejifunza tabia hiyo kutoka nyumbani au kwenye mazingira ya karibu na huifanya kama njia ya kuonesha hasira, kukata tamaa au kukosa udhibiti wa kihisia,” alisema.

Alieleza kuwa katika saikolojia ya mtoto, maadili na nidhamu hujengwa hatua kwa hatua kuanzia umri mdogo, yakikosekana mtoto hukosa mipaka ya kutambua lipi ni sahihi na lipi si sahihi.

Alisema watoto wanaokosa uangalizi wa karibu wa wazazi au wanaolelewa katika mazingira yenye mivutano, lugha chafu au ukosefu wa mawasiliano chanya, huwa katika hatari kubwa ya kuonesha tabia zisizokubalika wanapokabiliwa na shinikizo, ikiwemo mitihani.

Kwa upande wake Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Mkoa wa Mbeya, Magdalena Ngenzi, alisema matukio ya watoto kuandika matusi katika mitihani ya taifa yanaashiria pengo katika malezi shirikishi kati ya familia, shule na jamii.

Alieleza kuwa mtoto hukua ndani ya mifumo mitatu muhimu, nyumbani, shuleni na katika jamii, endapo mfumo mmoja utalegalega, mtoto huathirika kitabia na kimaadili.

“Familia inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kumlinda mtoto dhidi ya mienendo mibaya kwa kumpa malezi yenye maadili, uangalizi na mfano bora wa kuigwa,”.

Pia, alisisitiza umuhimu wa wazazi kusikiliza changamoto za watoto wao, kuwapa msaada wa kihisia na kuwajengea kujiamini, badala ya kuwasukuma kwa hofu au vitisho vinavyoweza kuongeza msongo wa mawazo.

“Hatua za malezi, ushauri na ulinzi wa mtoto zinapaswa kupewa kipaumbele ili kumsaidia mtoto kubadilika na kujenga maadili mema, hatua itakayosaidia si tu kuzuia matukio ya utovu wa nidhamu katika mitihani, bali pia kujenga jamii yenye watoto wenye maadili, heshima na uwajibikaji,” alisema.

SERIKALI

Hivi karibuni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima, aliwataka wazazi na jamii kwa ujumla kuwekeza katika malezi, makuzi na mawasiliano ya karibu na watoto ili kutambua mapema dalili za watoto wanaoelekea kuchukua maamuzi hatarishi.

Alisema changamoto nyingi zinazowakumba watoto zinatokana na kukosekana kwa muda wa wazazi kuwasikiliza na kuzungumza nao, hali inayowaacha watoto wakibeba mizigo ya kihisia bila msaada.

“Tunajiuliza watoto wamelala, lakini hatujiulizi wamekutana na nini mchana, nani amezungumza nao, au wamebeba hasira zipi. Tunatenga siku ngapi kwa wiki au mwezi kuzungumza na watoto wetu?” alihoji.

Waziri huyo alisisitiza kuwa malezi ya awali, hasa katika umri wa kuanzia miaka sifuri hadi mitano, ndiyo msingi wa kujenga imani kati ya mtoto na mzazi.

Alieleza kuwa tafiti zinaonesha kuwa katika kipindi hicho, ubongo wa mtoto hukua kwa kiwango kikubwa, na ndipo mtoto hujifunza kumuamini na kumsikiliza mlezi wake.

“Ukichelewa kuwekeza katika malezi, unakuja kupambana na mtoto akiwa na umri wa miaka 12 au 13, wakati tayari ameshajengewa mwelekeo tofauti na mazingira ya nje,” alisema.

Dk. Gwajima alibainisha kuwa baadhi ya watoto hupitia changamoto za kitabia au afya ya akili, jambo linalohitaji msaada wa kitaalamu badala ya lawama.

Previous Post

UPANDIKIZAJI MIMBA WARUDISHA TABASAMU KWA WANAWAKE NCHINI

Next Post

YANGA, AZAM FC FAINALI YA KIBABE

Next Post
YANGA, AZAM FC FAINALI YA KIBABE

YANGA, AZAM FC FAINALI YA KIBABE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MIAKA 64 YA UHURU YAWAIBUA BAYI, RAGE

MIAKA 64 YA UHURU YAWAIBUA BAYI, RAGE

5 months ago
‘MSAUZI’, MHISPANIA WACHUANA UKOCHA SIMBA

‘MSAUZI’, MHISPANIA WACHUANA UKOCHA SIMBA

5 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?